Skip to main content

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.




Moja kati ya elimu muhimu kwa kila mtu ambaye ameamua kufanya biashara ni elimu ya USIMAMIZI WA FEDHA. Fedha inahitaji usimamizi wa hali ya juu ili iweze kuongezeka na kutimiza malengo ulionayo katika biashara yako.

Unapokosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha inaweza kuzalisha matatizo kadha wa kadha katika biashara yako. Baadhi ya matatizo yanayoweza kutokea kwenye biashara yako kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri wa fedha.

Unaweza kupata hasara katika biashara yako.
Unaweza kupunguza kiasi cha mtaji wako.
Unaweza kuingia kwenye mgogoro wa madeni.
Unaweza kushindwa kununua mali ghafi kwaajili ya uzalishaji.
Unaweza kupoteza thamani ya jina la biashara yako.
Unaweza kupunguza thamani ya ubora wa bidhaa zako.

Kuna matatizo lukuki ambayo yanaweza kujitokeza kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha hivyo elimu ya masuala ya usimamizi wa fedha ni muhimu sana katika biashara yako.

Usimamizi wa fedha ni nini ?

Usimamizi wa fedha ni namna ya kusimamia mapato na matumizi katika biashara ili kutimiza lengo fulani.

Mapato ni fedha inayoingia katika biashara yako kupitia mauzo.

Matumizi ni fedha inayotoka katika biashara yako kupitia malipo.

Biashara yoyote ni lazima iwe na lengo (objective) ili uweze kuwa na ufanisi katika hiyo biashara. Huwezi kuwa makini katika biashara kama hujui unahitaji kutimiza nini.

Mpango kazi wa biashara ( Business Plan) ni kitu cha muhimu sana kwa kila mfanya biashara ambaye anataka kuleta mageuzi makubwa katika uchimu wake binafsi na jamii inayomzunguka.

Unapoweka kwenya matendo elimu ya usimamizi wa fedha inatakusaidia kutimiza malengo ulinayo katika biashara yako.

Kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kutengeneza mfumo wa usimamizi wa fedha katika biashara yako.

1. BAJETI ni mpango wa kifedha unaonyesha makisio ya mapato na matumizi katika biashara ndani ya kipindi fulani.

Katika bajeti kuna vipengele viwili vya muhimu ambavyo unapaswa kujua kwa kina ili uweze kutengeneza bajeti yenye kukidhi vigezo.

i/ Mapato
ii/ Matumizi
iii/ Muda maalum.

MAPATO; Mapato katika baishara hutokana na mauzo ya bidhaa au huduma. Kama unaona mapato yako ni kidogo katika biashara yako fikiria ni bidhaa gani au huduma gani ambayo unaweza kuongeza ili kuongeza mauzo katika biashara yako, unapoongeza mauzo moja kwa moja utaongeza mapato na kiasi cha faida.

Kwa mfanyabiashara anayeanza biashara ni vema ukajua chanzo cha mtaji wako ni nini ili kukusaidia kufanya makadirio vizuri.


MATUMIZI; Matumizi hutokana na malipo unayofanya katika biashara yako mfano kununua malighafi, kulipia pango kwaajili ya baishara, kuwalipa wafanyakazi, kulipia usafari kwaajili ya kusafirisha bidhaa nk.

Unatakiwa kuainisha matumizi ya baishara yako vizuri na ni vema ukatofautisha matumizi yako binafsi na matumizi ya biashara.

Changamoto kwa wafanyabaishara ni kuchanganya matumizi yao binafsi na matumizi ya biashara mfano unakuta mtu anatao fedha ya kununulia simu binafsi kutoka kenye baishara halafu baadae anajiuliza kwanini baishara yake haikui.

Unapotoa fedha kwenye biashara kwa matumizi binafsi bila kurudisha tarajia mambo haya kutokea kwenye biashara yako.

Faida kupungua.
Mtaji kupungua
Kupata hasara.

MUDA MAALUM; Ni lazima bajeti iandaliwe ndani ya muda maalum au kipindi fulani. Bajeti inaweza kuandaliwa kwa juma, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na hata mwaka mzima.

Bajeti inaonyesha makadiro ya mapato ndani ya kipindi fulani hivyo unakuwa na taswira ya mapato ya baishara ndani ya huo muda maalum.

Itandelea sehemu ya pili.

Imeandaliwa na

James Albert
Barua pepe jamesalbert157@gmail.com
+255757 471 244

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z