Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

           


Utangulizi 


MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani.

Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi.

Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha.Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo .Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii.


Tafiti zinaonyesha asilimia 60  ya faida ya benki hutokana na mikopo hivyo benki zipo makini sana na huduma ya utoaji mikopo kwa wateja wao ili ziweze kutengeneza faida kubwa. Watu wengine wamekuwa na mitazamo hasi juu ya huduma ya mikopo katika taasisi za kifedha kwasababu ya matokeo mabaya ya baadhi ya ndugu na jamaa zao kuchukuliwa mali zao kwa kushindwa kurejesha mikopo hiyo . Kihualisia mikopo ni moja ya njia nzuri na yenye tija katika kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika jamiii au maisha ya mtu mmoja mmoja .Mkopo ni njia moja wapo ya mtu kupata mtaji kwa ajili ya kufanya biashara kwa dhumuni la kuongeza kipato na kisha kufanya shughuli mbali za kimaendeleo.

Mambo ya msingi kufahamu kabla ya kuchukua mkopo katika taasisi za kifedha (benki ,mifuko ya hifadhi ya jamii na makampuni ya mikopo/Credit Company).


1.Dhumuni lako ni nini

Ni vizuri ukajihoji binafsi unachukua mkopo kwaajili ya kufanyia nin? Ni jambo la ajabu na la kusikitisha endapo utachukua mkopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida mfano kununulia nguo,chakula na kadhalika.Ni vizuri ukachukua mkopo kwa dhumuni la kufanyia biashara yaani chukua fedha ili uzalishe fedha,chukua mkopo kununulia thamani isiyoweza kuhamishika mfano kununua kiwanja ,kununua nyumba.

2.Je ni kiwango gani cha fedha kinaweza kukidhi haja ya biashara yako au thamani unayohitaji kununua

Pia ni jambo la msingi kujua unahitaji kiwango gani cha fedha kwasababu hata unapokwenda katika taasisi za kifedha kama benki na saccos moja katika ya swali muhimu ambalo utaulizwa ni kiwango gani cha fedha unahitaji? Ni vizuri kuwa na mpango kazi(Business Plan) wa biashara yako ambayo imebeba mchanganuo wa biashara yako kwa kina kiasi kwamba mpango kazi wenyewe uwe na uwezo wa kujibu maswali mengi ambayo taasisi za kifedha zitakuuliza.

3.Je unathamani ambayo unaweza kuweka rehani kulinda huo mkopo endapo utashindwa kulipa?( mfano wa thamni hizo ni Nyumba ,kiwanja au shamba)

Taasisi za kifedha huwa wanahitaji uwe na thamani ya kuweka rehani kwa ajili ya mkopo unaotaka kuchukua ili fedha zao ziwe katika mazingira salama endapo utashindwa kulipa .Kwa watu ambao ni waajiriwa huwa inahitajika barua ya mwajiri na pia awe mteja wa benki husika mwenye akaunti ya mshahara katika hiyo benki.Kuna baadhi ya taasisi za kifedha ambazo zinaweza kukupa fedha bila kuwa mteja kwao lakini ni lazima udhaminiwe na mteja ambaye ana akaunti katika taasisi husika.

4.Je unauwezo wa kurejesha mkopo kwa muda gani? 

Ni vizuri kufahamu kipindi ambacho fedha hiyo inapaswa kurudi katika taasisi husika ili ujue kama kwa kipindi hicho utakuwa na uwezo wa kulipa mkopo huo .Unapokwenda katika taasisi za kifedha kwa dhumini la kuchuka mkopo ni vizuri ukauliza muda wa kuanza kulipa mkopo huo na je ni kiwango gani unapaswa kulipa mkopo huo kwa mwezi  mpaka utakapo kwisha.

5.Je mkopo huo unariba ya kiwango gani?

Mara nyingi taasisi za kifedha huwa wanahitaji kukopesha wakati riba ikiwa  juu na wao kukopa wakati riba ikiwa ndogo  .Kwa taratibu za kibenki na fedha wakati mzuri wa kukopa ni kipindi ambacho kiwango cha riba kikiwa chini lakini swala hili katika nchi yetu mara nyingi riba imekuwa katika kiwango fulani bila kubadilika hivyo unachopaswa ni kujua kiwango cha riba ambacho kinatozwa na taasisi husika kabla ya kufanya maamuzi ya kukopa.



By James Albert 

Comments

  1. Unatafuta kampuni halisi ya mkopo wa kifedha ili kupata mkopo wa euro 10,000 hadi euro 10,000,000 (kwa mikopo ya biashara au biashara, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya nyumba, mikopo ya gari, mikopo ya uimarishaji wa madeni, mikopo ya mtaji wa mradi, mikopo ya afya nk. ))Au ananyimwa mkopo kutoka benki au taasisi ya fedha kwa sababu yoyote ile?Tuma ombi sasa na upate mkopo halisi wa kifedha. Imechakatwa na kuidhinishwa ndani ya siku 3. PACIFIC FINANCIAL LOAN FIRM

    Sisi ni wakopeshaji wa mkopo wa kimataifa ambao hutoa fedha halisi kwa watu binafsi na makampuni kwa riba ya chini ya 2% tukiwa na kitambulisho halali au pasipoti ya kimataifa ya nchi yako ili kuthibitishwa. Malipo ya mkopo huanza saa 1 (moja) baada ya mkopo kupokelewa. na muda wa kulipa ni miaka 3 hadi 35.

    Kwa jibu la haraka na kushughulikia ombi lako la mpaka ndani ya siku 2 za kazi
    Wasiliana nasi moja kwa moja kupitia barua hii: pacififinancialloanfirm@gmail.com

    Wasiliana nasi kwa maelezo yafuatayo:

    Jina kamili: ____________________________
    Kiasi cha pesa kinachohitajika kama mkopo: _______________
    Muda wa mkopo: ___________________________________
    Madhumuni ya mkopo: ____________________
    Siku ya kuzaliwa: ___________________________________
    Jinsia: ______________________________
    Hali ya Ndoa: ___________________________________
    Anwani ya mawasiliano: ___________________________________
    Mji / Msimbo wa Eneo: ___________________________________
    Nchi: ______________________________
    Kazi: ___________________________________
    Simu ya rununu: __________________________

    Tuma ombi lako la jibu la haraka kwa: pacififinancialloanfirm@gmail.com
    asante

    Afisa Mtendaji Mkuu :Pen Fed VICTORIA JOHNSON

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.