Changamoto walionayo watu wengi
sio kuanzisha biashara au kuanzisha kampuni bali ni kuanzisha biashara gani au
kampuni gani,kuna watu wanafedha lakini hawajui wafanye nini na fedha hizo. Watu wengi wamekutana
na changamoto hii ya kupata wazo la
biashara kiasi ambacho wamekuwa wakitamani kufanya biashara lakini hawajui ni
biashara gani haswa wanapaswa kufanya.
Napenda kukukaribisha kwa moyo
mkunjufu katika kusoma makala hii ambayo
nitaeleza kwa uchache baadhi ya njia za kupata wazo la biashara au kuanzisha Kampuni.
CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA JAMII
UNAYOISHI
Chunguza katika jamii unayoishi
je kuna changemoto gani au zipi na je kupitia changamoto hizo unaweza kufanya
biashara gani au kuanzisha kampuni gani ambayo bidhaa zake zitakuwa ni suluhu ya
hiyo changamoto katika jamii husika. Njia hii mara nyingi inakupa uhakika wa
soko la bidhaa zako na huduma utakayotoa kwa wananchi. Kusudi la njia hii ni
kutatua changamoto inayokabili jamii husika wakati ukiendelea kujiingizia
kipato.
Mfano I:- Katika kijiji cha WATANZANIA TUMEAMUA kuna changamoto
ya upatikanaji wa maji safi na salama hivyo unaweza kuchimba kisima na
kuanzisha biashara ya kuuza maji kwa wanakijiji.
Mfano II:- Katika kijiji cha KILA
MTU ANA THAMANI kuna changamoto kubwa ya
upatikanaji wa usafiri hivyo unaweza kuanzisha huduma ya kutoa usafiri wakati
huohuo unajitengenezea kipato.
Mfano III:- katika mtaa wa HEKIMA kuna changamoto ya upatikaji wa sehemu ya kula kwa wafanyakazi wa kiwanda
cha TANZANITE YETU hivyo unaweza kuja kufanya biashara ya kuanzisha mgahawa na
kuuza chakula kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho na wanajamii wengine.
Mfano IV:- Katika kijiji cha
MAARIFA YA MAISHA kuna changamoto ya upatikani wa bidhaa za matumizi ya nyumbani
hivyo wananchi wanasafiri umbali mrefu kwenda kununua bidhaa hizo, hivyo basi kupitia chanagamoto hii unaweza kuanzisha baishara ya kuuza duka.
Mfano V:- Katika mtaa wa ELIMU NI
MUHIMU kuna changamoto ya upatikanaji wa
mahitaji ya sokoni mfano nyanya ,vitunguu ,matunda n.k hivyo unaweza kuanzisha
biashara ya kuuza bidhaa hizo katika eneo zuri na safi ambalo litawavutia
wateja kuja kununua bidhaa zako.
MUHIMU
Tafiti ni muhimu sana kabla ya kuazisha biashara yoyote ile, hivyo basi ninashauri ufanye utafiti wa kina juu ya eneo unaloishi ilikujua changamoto ambazo zinakabili jamii
inayokuzunguka na kisha kuja na mpango mkakati wa kuanzisha biashara ambayo
inakuwa suluhu ya hizo changamoto wakati wewe unajiingizia kipato.
Itaendelea sehemu ya pili
Imeandaliwa na James Albert
SOMO ZURI SANA SANA
ReplyDelete