Umuhimu wa tovuti/mtandao kwa biashara ndogo.


Katika ulimwengu wa leo kupatikana au kutokupatika kwa biashara yako katika mtandao wa internet kutaathiri  kiasi cha mafanikio utakayopata. Ni muhimu kila mmiliki wa biashara  kuwezesha biashara yake kupatikana na kuonekana mtandaoni kwa kupitia tovuti za kompyuta,simu au kurasa za mitandao ya jamii.  Mtandao wa internet  unatakiwa uwe nguzo na nyenzo muhimu sana katika mkakati wako wa kutangaza biashara au bidhaa.
Katika sehemu ya kwanza ya makala hii nitaonyesha umuhimu wa mfanyabiashara au mtu binafsi kumiliki tovuti. Tovuti nzuri ina uwezo mkubwa wa  kuipa biashara yako thamani na kukutofautisha na  washindani wenzako katika soko la bidhaa na huduma.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kumiliki tovuti na kuitumia kama chombo cha kufanya biashara na  kujitangaza.


Tovuti itafanya biashara yako iaminike zaidi.

Katika kizazi hiki  watu wengi zaidi hutegemea mtandao wa internet kutafuta taarifu kuhusu bidhaa au huduma flani kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Biashara yako itanufaika mno kama itakua inapatikana kwa urahisi mtandaoni. Bila tovuti wateja wengi hasa vijana watafanya manunuzi  kwa washindani wako ambao taarifa zao zinapatikana mtandaoni.


Utajitangaza saa 24 kila siku kwa gharama kidogo kuliko njia  nyingine za kawaida za matangazo.

Gharama ya kutengeneza tovuti hutofautiana kulingana na mtengenezaji lakini punde tovuti itakapo kamilika, itakupa wewe na biashara yako uwezo wa kujitangaza kila saa sababu tovuti hupatikana hewani muda wote,wakati wowote na mahali popote ulimwenguni. Njia za kawaida za kujitangaza kama redio,magazeti na TV zinagharama kubwa mno. Tovuti iliyotengenezwa vyema  ni  moja kati ya njia rahisi zaidi na ya gharama nafuu zaidi ya  kutangaza biashara yako katika kizazi hiki  kinachotegemea mtandao.

Tovuti ni kipeperushi chako cha mtandaoni.

Tovuti ni kipeperushi kinachoelezea biashara yako ambacho kinaweza onekana mahali popote  duniani. Vipeperushi vya kawaida huchanika na kuharibika baada ya muda lakini tovuti  huzidi kuonekana pasipo kujali ilitengenezwa lini. Tovuti pia ni njia rahisi ya kuwataarifu wateja wako kuhusu bidhaa mpya,promosheni au huduma  mpya.

Urahisi kwa wateja wako

Tovuti huwapa wateja wako urahisi mkubwa, kwa sababu wanaweza wakatafuta/kugundua bidhaa na huduma ulizonazo wangali nyumbani au ofisini mwao pasipo kuingia gharama ya kusafiri hadi dukani mwako.  Urahisi huu  huwasaidia wateja wako kuokoa gharama na hivyo kuvutiwa zaidi kufanya biashara na wewe. Wateja huvutiwa kwa sababu miundo mbinu yako  huwasaidia kupunguza gharama ambazo wangekabiliana nazo kutembelea duka lako ili kujua huduma na bidhaa zipatikanazo. Swala hili litakupa upendeleo machoni pa wateja kuliko wenzako wasio na miundo mbinu ya mtandaoni.


Uwezo wa kufanya biashara popote nchini na ulimwenguni.


Tovuti hupatikana popote ulimwenguni, kwa hivyo unaweza kupata wateja popote pasipo kujali mipaka ya kijiografia. Unachotakiwa kufanya ni kutoa huduma na bidhaa ambazo ni bora kuliko washindani wengine katika soko husika.   
Ni muhimu SANA kwa mmiliki wa biashara kutengeneza tovuti au ukurusa katika mitandao ya kijamii kwani uwepo wako mtandaoni  utachangia sana kukuza kipato chako hasa katika bidhaa na huduma zinazotumika na vijana.

***
Tunaweza kutengeneza  tovuti kwa ajili ya biashara yako. Wasiliana nasi kwa:
Simu: +255 767 840 494.
Barua pepe: info@webconsulting.co.tz

Nakutakia mafanikio!

Comments

Popular posts from this blog

Namna Ya Kuanzisha Biashara

Biashara Ya Mbao.

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.