MUONGOZO WA KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASIRIMALI

  SEHEMU YA KWANZA

Na; James Albert 




Ni jambo la burasa kuwa na vikundi vya wajasiamali wadogowadogo kwa lengo la kuunganisha nguvu pamoja lakini pia kuweza kupata fursa mbalimbali zilizopo katika mfumo wa uchumi.

Kabla ya kutoa muongozo wa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali napenda kutoa sababau za kwanini ni vizuri kuwa katika mfumo wa kikundi

i)  Ili kuweza kupata msaada ya kitaalamu na kimtaji katika serikali ni lazima kuwa katika mfumo wa kikundi.
ii)  Ni rahisi kupata mtaji kwasababu katika kikundi mtaji unachangiwa na wanachama wote lakini ingekuwa mtu mmoja kitendo cha kukusanya mtaji kinaweza kuchukua muda mrefu pia taasisi za kifedha kama mabenki wanatoa mikopo katika kikundi na sio mfanya biashara mdogo mojamoja kwasababu kikundi ndio kinakuwa dhamana ya mkopo. 
iii) Ni rahisi kupata mafunzo kutoka katika  mashirika yasiyo ya kiseriakali na serikali kwa ujumla na rahisi serikali kuhusika na suala la kikundi kuliko mtu mojamoja. .
iv) Kuna uwezekano na kuwa na mtaji mkubwa katika kikundi andapo wajisiriamali wote wataamua kuunganisha mitaji yao midogo.
v) Ni rahisi kupata wataalamu wa masuala ya mbalimbali katika kikundi kwasababu wanachama wake ni watu wenye taaluma na uzoefu tofauti. 
vi) Unapokuwa katika mfumo wa kikundi inapunguza ukubwa wa harasa katika biashara. Mtu akiwa anafanya biashara pekee kiwango cha hasara anachoweza kupata ni tofauti na hasara ya kikundi. 

Itaendelea sehemu ya pili
Imeandaliwa na 
James Albert
barua pepe jamesalbert157@gmail.com
Simu +255717162510

Comments

Popular posts from this blog

Namna Ya Kuanzisha Biashara

Biashara Ya Mbao.

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.