Suala la huduma kwa mteja ni muhimu katika biashara lakini kuwajali wateja ni muhimu zaidi kwasababu ni suala lenye kujenga mahusiano ya kibiashara kwa muda mrefu. Huduma kwa mteja (Customer service) ni kitendo cha kumsaidia mteja kukamilisha muhamali fulani lakini kumjali mteja (Customer care) ni kitendo cha kumuwezesha mteja kukamilisha muhamala fulani na kumfanya mteja aweze kurudi tena kununua biadhaa au hudumu.
Je wewe ni mmoja wa watu ambao umewahi kwenda katika duka fulani ukajibiwa vibaya na muuza duka wakati ukiulizia bei ya bidhaa fulani au umewahi kufika dukani wa kwanza halafu wakaja wateja nyuma yako na wakahudumiwa wewe ukabaki, umewahi kumsalimia muuza duka na hakupokea salama yako?, umewahi kutofautiana na muuza bidhaa fulani akaanza kukutukana, kukukeji na kukuvunjia heshima? baadhi ni mambo ambayo watu wengi wamekutana nayo wakiwa wakinunua biadhaa au huduma fulani. Maswali hayo ni vitu ambayo kwa asilimia kubwa vinafukuza mteja asiweze kurudi kununua bidhaa yako na anapozungumza na watu wengine huwa anawashawishi wasije kununua hizo huduma kwako.
Tafiti zinaonyeshaa asilimia kuwa ya wateja wapya wa benki ni wateja ambao walishawishiwa kujiunga na huduma za kibenki kupitia ndugu na marafiki zao. Hii inamaana walipata huduma bora kwa kiasi cha kuweza kuwapendekeza (recommend) benki kwa marafiki zao lakini kama wasingepata huduma bora wasingeweza kuwashawishi marafiki zao.
Kama mjasiriamali ni vema ukafiri kujenga mahusiano ya kibiashara yatakayo dumu kwa muda mrefu kwa kila mteja unayepata fursa ya kukutana naye. Kujali mteja ni ujuzi unaoweza kujengwa ndani ya mtu ili aweze kufanya vizuri katika biashara aliyopo. Kuna makapuni mengi ambayo yamewekeza fedha nyingi katika mafunzo ya kumjali mteja kwa wafanyakazi wake ambao wanakutana na wateja katika shughuli za kila siku.
Comments
Post a Comment