NGUZO YA UBUNIFU

                                                       SEHEMU YA I 



Moja ya kitu ambacho kinaweza kumpa mjasiriamali nguvu ya kuteka soko la bidhaa au huduma fulani ni Ubunifu. Kimsingi huduma huduma na bidhaa nyingi tayari zimekuwepo sokoni kwa kipindi cha miaka kadha na ni nadra sana kuona mjasiriamali anakuja na bidhaa/huduma ambayo haijawahi kuwepo sokoni. 

Ubunifu ni hali au uwezo mpya wa kutoa huduma tofauti yenye ubora wa juu kuliko huduma iliyokuwepo sokoni au kuja na namna mpya ya kutoa huduma fulani ambayo ni tofauti wa wauzaji wengine wa bidhaa/huduma hiyo. 

Unaweza kukuta katika eneo moja kuna wauzaji wa nafaka wengine lakini kuna muuzaji mmoja ambaye ndiye mwenye wateja wengi kuliko wengine na ukichunguza utandua kuna kitu huyo mjasiriamali anacho ambacho wengine hawana kabisa kitu hicho. Inaweza kuwa ni kauli nzuri, namna nzuri ya kufunga mzigo (packagging), bei nafuu, usafi wa eneo, kutoa ziada ya huduma mfano unaweza kukuta mjasiriamali anauza mahindi na huduma ya ziada ni mteja kubebewa mzigo au kupewa mfuko wa kubebea bure. 


KUNA VITU VYA MUHIMU VINAVYOMUWEZESHA MJASIRIMALI KUWA MBUNIFU

1. KUWA NA UEKEKEO THABITI

Ni muhimu sana mjasirimali kujua anahitaji kufanya nini katika biashara yake kabla hata ya kuanza hiyo biashara ili aweze kujua anapaswa kuwekeza kwenye nini, afanye biashara yake kwenye eneo gani, anampango wa kuwa na wateja wa aina gani, anahitaji kuuza huduma/bidhaa gani na mengine mengi. Kuwa na uelekeo thabiti inamsaidia mjasirimali kuwa na msingi mzuri wa kufanya maamuzi yenye tija na kuleta matokeo chanya katika biashara yake. 


2. KUTAFUTA MBADA WA HUDUMA/BIDHAA

Katika maisha yetu kuna biashara mbalimbali ambazo tayari zipo ili mjasirimali aweza kuwa na huduma bora anapswa kufanya uchunguzi wa bidhaa zilizopo zinaupungufu gani au kuna ombwe(gap) kati ya matarajio ya wateja na huduma inayotoletwa baada ya kubaini huo upungufu ni hekima kuja na biashara ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa huduma bora na kwa namna ya kipekee ukilinganisha wa na huduma za wajasiriamali wengine waliopo sokoni. 

Itaendelea Sehemu ya II 

Imeandaliwa na James Albert 

Namba ya whatsapp 0717165210

Barua pepe jamesalbert157@gmail.com 


Comments

Popular posts from this blog

Namna Ya Kuanzisha Biashara

Biashara Ya Mbao.

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.