Kupitia blog unaweza kuijingiza kipato kizuri sana ikiwa kazi hii utaifanya kwa ubora wa hali ya juu.
Kuanzisha blog yenye kuingiza kipato mtandaoni linaweza kuwa jambo geni na la kushangaza kwa baadhi ya watu kwasababu huenda hawajawahi kujua namna blog inavyoweza kuingiza kipato.
Ukweli ni kwamba nimefanya blogging kwa kipindi cha muda wa miaka 7 lakini nilipoanza mwaka wa 8 ndio nilianza kutafuta namna ya kuingizia kipato. mtandaoni
Baada ya kujifunza namna nilivyoweza kujifunza kuingiza kipato kupitia blog mtandaoni nimeona ni vyema nikushirikishe na wewe.
Mentor wangu kwenye Blog Ally Msangi aliwahi kusema “Blogging ni biashara ambayo ukifanya serious inalipa vizuri sana”
Hii ni moja ya kauli ambayo ilinifanya kugeuza mtazamo wangu kwa kiasi kikubwa kwenye masuala ya Blogging.
Je Blogging ni nini ?
Blogging ni kitendo cha kutengeneza maudhui na kuyachapisha katika mtandao wa intaneti.
Kuanza biashara ya Blogging inaweza kuwa jambo gumu lakini ukiwa na ushauri wa kitalamu ni jambo linalowezekana.
Unapofikiria kuanza biashara ya Blogging ni lazima uweke akili yako kujifunza ni suala endelevu na hii ni kwasababu mambo yanabadilika sana kulinga na maendeleo ya teknolojia.
Kupitia blog unapata fursa ya kuingiza kipato kupitia blog
Mambo ya Kuzingatia
i. Chagua jambo unahitaji kuandika kuhusu nini kwenye Blog, ukweli ni kwamba ukiweka kama mtaalamu blog yako itafanya vizuri sana.
Mfano unaweza kuamua kwenye blog yako uandike kuhusu afya, biashara, malezi ya vijana, ajira, ufugaji wa paka au jambo lingine.
Ukichagua jambo moja ambalo utakua unaandika mada mbalimbali itakusaidia wasoma wako kujua uko focused na unaeleza kitu ambacho unakijua.
Mfano Daktari wa binadamu ni mtaalamu lakini Daktari wa ngozi ni mtaalamu zaidi na anaheshimika kuliko daktari anaye tibu magonjwa yote.
Kwenye blogging chagua jambo ambalo utaliandikia vizuri na kwa weledi wa hali ya juu.
ii. Chagua jina la blog yake ambalo litakua rahisi na wazi kwa wasomaji wako, epuka kutumia maneno magumu sana ili iwe rahisi kwa mtu kukumbuka jina la blog ikiwa anahitaji kufanya rejea ya alichosoma.
iii. Chagua kampuni ya kununua domain na hosting. Yapo makapuni mengi yanayofanya biashara ya kuuza domain name na kuhost hivyo fanya utafiti kujua ni kampuni ipi inaweza kukidhi mahitaji yako. Ingawa inashauriwa ununua domain kwingine na hosting ufanye kwingine ili kuongeza usalama wa taarifa zako kama inatokea changamoto.
Endendelea kutembelea tovuti hii kwa maarifa zaidi.
Comments
Post a Comment