Kuongeza thamani katika biashara ni kitu muhimu kwaajili ya ukuaji na mafanikio ya biashara yako kwa ujumla.
Thamani katika ulimwengu wa biashara inamaanisha ubora wa bidhaa/huduma kutoka na umuhimu wake ukilinganisha na pesa anayolipia mteja.
Biashara ambayo inatoa thamani kwa wateja wakati ni biashara ambayo itavutia wateja sana.
Unaweza kuongeza thamani katika biashara kwa kutumia njia mbalimbali lakini wewe kama mjasiriamali unahitaji kujua ni njia ipi ni sahihi katika biashara yako.
Njia za kuongeza thamani
Kuwajali wateja
Kuwajali wateja ni njia moja wapo ya kuongeza thamani katika biashara.
Wateja wanathamani na kupenda biashara ambayo inaridhisha zaidi ya mahitaji yao.
Hii inafanyika kwa kujifunza namna ya kuwajali wateja, kufanyia kazi malalamiko ya wateja, kutoa mrejesho wa wakati, kugusa hitaji la mteja wakati unamuhudumia.
Mara nyingi wateja wakijaliwa vizuri huwa wanawaambia watu wengine kuhusu ubora wa huduma na bidhaa zako. jambo ambalo huongeza mauzo na mapato katika biashara.
Njia nyingine ya kuongeza thamani katika biashara yako ni kutoa huduma/bidhaa bora kwa wateja.
Wateja huwa wako tayari kulipia huduma/bidhaa ambazo zina ubora wa hali ya juu.
Unaweza kutumia malighafi zenye ubora kutengenezea bidhaa zako au kutumia watu wenye ujuzi kutengeneza bidhaa.
Ukitengeneza bidhaa zenye ubora itakusaidia kujitofautisha na wafanyabiashara wengine sokoni.
Kuboresha urahisi
Hii inaweza kufanyika kupitia huduma au biashara kupatikana kwa urahsi, kufungasha bidhaa vizuri na (faster delivery) kupeleka kwa wateja kwa wakati.
Wateja wanapoona unafanya delivery kwa wakati, umefunga bidhaa vizuri huamini hiyo bidhaa ina thamani.
Kumshauri Mteja
Kabla ya mteja kununua bidhaa unamueleza manufaa ambayo atapata akinunua hiyo bidhaa.
Mteja akishanunua bidhaa unamshauri namna nzuri ya kutumia bidhaa au huduma ili apate manufaa zaidi.
Kumshauri kunaweza kuwa sambamba na matunzo ya hiyo bidhaa
Mfano Mteja amenunua simu unamueleza namna bora ya kutunza betri ya simu yake ni kuepuka kuchaji simu wakati anatumia.
Kuchaji simu wakati amepokea notification kuwa betri ni low na sio kuchaji tu simu wakati wowote.
Mwisho, mfanya biashara ambaye anathamini biashara yake wateja wake wataithamini hiyo biashara.
Comments
Post a Comment