Mambo muhimu kuhusu mikopo kabla ya kuchukua mkopo katika taasisi za kifedha.
Zifuatazo ni dondoo muhimu kuhusu mikopo.
1.Dhumuni lako ni nini
Ni vizuri ukajihoji binafsi unachukua mkopo kwaajili ya kufanyianin?.
Jambo la ajabu na la kusikitisha endapo utachukua mkopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida mfano kununulia nguo,chakula na kadhalika.
Chukua mkopo kwa dhumuni la kufanyia biashara yaani chukua fedha ili uzalishe fedha.
2.Je ni kiwango gani cha fedha kinaweza kukidhi haja ya biashara yako au thamani unayohitaji kununua
Unahitaji kiwango gani cha fedha unapokwenda katika taasisi za kifedha kama benki na saccos moja kati ya swali muhimu ambalo utaulizwa ni kiwango gani cha fedha unahitaji?.
Awali, kuwa na mpango kazi(Business Plan) wa biashara yako ambayo imebeba mchanganuo wa biashara yako kwa kina.
Mpango kazi wenyewe uwe na uwezo wa kujibu maswali mengi ambayo taasisi za kifedha zitakuuliza.
3.Je unathamani ambayo unaweza kuweka rehani kulinda huo mkopo endapo utashindwa kulipa?( mfano wa thamni hizo ni Nyumba ,kiwanja au shamba)
Taasisi za kifedha huwa wanahitaji uwe na thamani ya kuweka rehani kwa ajili ya mkopo unaotaka kuchukua ili fedha zao ziwe katika mazingira salama endapo utashindwa kulipa.
Kwa watu ambao ni waajiriwa huwa inahitajika barua ya mwajiri na pia awe mteja wa benki husika mwenye akaunti ya mshahara katika hiyo benki.
Tena baadhi ya taasisi za kifedha ambazo zinaweza kukupa fedha bila kuwa mteja kwao lakini ni lazima udhaminiwe na mteja ambaye ana akaunti katika taasisi husika.
4.Je unauwezo wa kurejesha mkopo kwa muda gani?
Ni vizuri kufahamu kipindi ambacho fedha hiyo inapaswa kurudi katika taasisi husika ili ujue kama kwa kipindi hicho utakuwa na uwezo wa kulipa mkopo huo. .
Unapokwenda katika taasisi za kifedha kwa dhumini la kuchuka mkopo uliza.
Comments
Post a Comment