Nichi Ya Soko

 Nichi ya soko kwaajili ya biashara ni suala la msingi kwaajili ya ustawi wa biashara yako

Kwa maneno mengine ni eneo maalamu la soko ambalo linakua na bidhaa/huduma maalumu.

Ina maanisha  kipande cha soko ambacho kina mahitaji tofauti, sifa na machaguo tofauti ya wateja.

Kipande hiki cha soko kinaweza kubainishwa kwa kutumia vigezo mbalimbali.

Mfano tabia za watumia huduma, mtindo wa maisha wa watumia huduma, eneo ambalo watumia huduma hupatikana

Katika soko kubwa ndani yake kuna masoko madogomadogo mfano soko la viatu, nguo, matunda, vifaa vya umeme na masoko mengine.

Mfano biashara ya suruali za jinsi hii ni nichi kamili.

Nichi hii inaelezea bayana watumiaji kwa asilimia kubwa watakuwa ni vijana wenye umri kati ya miaka 18-35 kwasababu umri huo ndio kuna vijana.

Pia ni kundi ambalo linabadilika  kwa urahisi kulingana na mtindo na wakati.

Mfanyabiashara anaye chagua nichi ya suruali za  jeans ni lazima awe ni mtu ambaye anafuatilia matulio ya jeans mpya kulinga na mtindo mpya kila wakati.

Umuhimu wa Nichi 

Suala la kuchagua nichi ya soko ni muhimu kwaajili ya mafanikio ya biashara. Zifuatazo ni sababu za kwanini uchague nichi ya soko .

Kiwango kidogo cha usindani.

Uchaguzi wa nichi mzuri  hupunguza ushindani kuliko ushindani ambao ungepatikana katika soko kubwa kadri unavyochagua  soko la bidhaa zako ndivyo unavyopunguza ushindani wako sokoni.

Unalenga soko la bidhaa, kwa kuchagua nichi sokoni inakusaidia kulenga kutoa bidhaa mahususi kwa wateja wako ambao unajua sifa zao.

Hii inakusaidia wateja kujua kujua chapa au jina la bidhaa zako kwa urahisi sana.

Faida kubwa, biashara ambayo imechaguliwa nichi nzuri inaweka uwezekano mkubwa wa kutengeneza faida kubwa,

Kwasababu bidhaa zinazokuja sokoni ni kulinga na mahitaji maalumu ya wateja wako hivyo huwezi kuleta bidhaa ambazo hazitauzika.

Utofauti wa chapa ya biashara, unapojikita kwenye nichi fulani sokoni inasaidia biashara kutofautishwa na biashara zingine zilizopo sokoni.

Chapa kutambulika sokoni inafanya watu kuwaelezea wengine kwa urahisi kuhusu biashara yako.

Mwisho,  mafanikio ya biashara yako yanategemeana na nihci sahihi hivyo inahitaji mkakati madhubuti kwaajili ya uchaguzi wa nichi nzuri na yenye tija.

Comments

Popular posts from this blog

Namna Ya Kuanzisha Biashara

Biashara Ya Mbao.

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.