Skip to main content

Kutengeneza Pesa Mtandaoni.



Kutengeneza pesa mtandaoni ni jambo ambalo linaweza kupunguza  changamoto ya upungufu wa fursa za ajira nchini.


Kila mwaka mamia elfu ya vijana wanahitimu kutoka katika vyuo vya kati na vyuo vikao na kuingia katika soko la ajira nchini Tanzania.


Mambo Muhimu Ya Kijana Kuzingatia ili Kutengeneza kipato mtandaoni.

Chagua unahitaji kufanya nini 


Ukweli ni kwamba huwezi kufanya kila kitu mtandaoni kwasababu fursa zipo nyingi sana.


Unahitaji kuchagua jambo ambalo unahitaji kufanya ili kutengeneza pesa mtandao.


Uchaguzi wako unatakiwa kutegemeana na utafiti ambao umeufanya ni ujuzi gani ambao unahitajika sokoni au ni bidhaa gani inahitajika sokoni


Mtaalamu wa mauzo ndugu Amos Nyanda anasema "Soko ni maabara hivyo halidanganyi"


Kumbuka huduma au bidhaa unayotaka kupeleka sokoni sio kwaajili yako hivyo ni busara soko liamue huduma gani au bidhaa gani inahitajika ili uweze kutengeneza pesa mtandaoni.


Kubali kujifunza


Ili uweze kuingiza kipato mtandao ni lazima uwe ni mtu ambaye uko tayari kujifunza kwasababu unaingia katika sehemu mpya. Jifunze namna mifumo inafanya kazi na kuleta matokeo yaani wekeza kwanza kujifunza utaratibu mzima wa mfumo wa mtandao husika.


Lakini mtandao ni sehemu ambayo mambo yanabadilika kila wakati.


Huwezi kukwepa mabadiliko hivyo namna pekee ya kwendana nayo ni kuamua kujifunza ili ukabiliana nayo.


Tafuta mtu wa kukuelekeza


Kuna watu ambao wapo kwenye mtandao kwa muda mrefu sana wanafanya jambo fulani mfano kwenye masuala ya blog ndugu Ally Msangi ni mtu ambaye anafanya masuala ya blogging kwa muda mrefu.


Hawa watu kwa jina lingine wanaitwa MENTORS .


Ni watu muhimu kwababu wanajua njia sahihi ambayo ukiipitia unaweza kupata matokeo mazuri.


Mentors ni watu wenye uzoefu wa kutosha kwasababu wanaishi jambo ambalo wanafundisha.


Usijifunze jambo kwa mtu ambaye yeye mwenye haishi hicho kitu mfano usijfunze masuala ya mauzo kwa mtu ambaye yeye sio muuzaji.


Ukijifunza kwa mentor itakupunguzia gharama ambayo ungeingia wakati unanunua vitabu na muda ambao ungetumia kujifunza huko mtandaoni kama YOUTUBE na majukwa mengine.


Kuwa mvumilivu 


Huwezi kuingia mtandaoni leo na ukaanza kutengeneza pesa mtandaoni wakati huohuo inachukua muda. Unahitaji kuwa mvumilivu wakati unafanya kazi mtandaoni ili uweze kupata matokeo unayotarajia tofauti na hivyo.


Mwisho, kijana wekeza muda kujifunza kabla ya kufanya jambo lolote itakusaidia kuepuka makosa mengi, kupoteza pesa na muda wako pia.


Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z