Kuingiza pesa mtandaoni katika nyakati hizi za mapinduzi ya teknolojia kumekuwepo na hamasa kubwa ya watu kutengeneza pesa kupitia mtandao wa inteneti jambo ambalo sio baya lakini linahitaji mpango madhubuti.
Kuingiza pesa mtandaoni inawezekana kabisa kupitia jitihada makusudu.
Ukweli ni kwamba sio jambo jepesi, inahitaji kuwa mbunifu, bidii na ujuzu wa namna ya kuingiza pesa.
Baadhi hapa chini ni namna ya kuingiza pesa mtandaoni
1. Namna ya kwanza unaweza kuingiza pesa kupitia blog kwa kuuza bidhaa ndani yake kama vitabu au course ambazo umetengeneza mwenyewe na kuuzia watu wengine.
2. Namna ya pili ni kuingia makubaliano na baadhi ya kampuni.
Hii itakupa fursa ya ili kutangaza bidhaa zao kupitia blog na wao wakakulipa commission fulani ambayo mmekubaliana nao ili uweze kuingiza pesa kupitia mtandao.
3. Namna ya tatu kuingiza pesa mtandaoni ni kutangaza aina ya huduma unayoweza kuwapa watu na wao waka tayari kulipia kupitia mtandao wako wa blog.
4. Unaweza ya nne ni kujisajili katika makujwa ya wafanayakazi huru (freelancer).
Majukwa hayo ni kama upwork, fiverr na mengine mengi kisha ukauza ujuzi wako huko na kujiingizia fedha za kutosha.
5. Unaweza kutengeneza akaunti za mitandao ya kijamii na kisha kujitangaza kwa kutoa huduma fulani.
Mfano kutengeneza matangazo ya biashara (Copy Writing), unaweza kuanda poster kwaajili ya watu kutangazia biashara zao.
6. Unaweza kutengeneza pesa kupitia kusimamia na kuandika maudhui kwenye akaunti za watu kwaajili ya kutangaza biashara zao.
Kujibu maswali yote ambayo wateja wao wanauliza kupitia mitandao ya kijamii ya biashara husika.
Jambo muhimu ni kujenga ujuzi ambao unahitaji kuufanyia kazi sokoni katika kuingiza kipato ili iwe rahisi kwako kupata wateja.
Kwenye majukwa ya mtandao wanahitajika watu wenye ujuzi.
Namna zote ambazo nimeendika zitakazokusaidia kuingiza pesa mtandaoni zinahitaji ujuzi fulani
Niandikie unatamani kujifunza kuhusu nini kwenye masuala ya ujasiriamali na biashara kwa ujumla.
Endelea kutembelea tovuti hiii kwaajili ya kujifunza zaidi kuhusu ujasiriamali na biashara.
Kwenye sehemu ya mitandao ya kijamii naomba nifollow ili uweze kupata mafunzo katika hizo sehemu pia.
Mwisho, suala la kufanya kazi mtandao ili kutengeneza kipato linahitaji uwekezaji, uvumilivu na kufanya kazi kwa bidii.
Comments
Post a Comment