Masoko ya mitandao ya kijamii ni mchakato wa kutengeneza na kushirikisha maudhui watu yenye lengo la kutangaza huduma/bidhaa yako kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi ya mitandao ya kijamii ni kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Threads na Truth Socia Media.
Lengo la masoko ya mitandao ya kijamii ni kuwajengea wateja uelewa.
Kuhusu huduma/bidhaa zako, kuongeza watembeleaji wa tovuti ya biashara na kuongeza mauzo kwa ujumla.
Masoko ya mitandao ya kijamii yanahitaji ufahamu wa hali ya juu kufikia wateja ambao umewakusudia.
Mfano wateja kusudiwa wanaweza kuwa wanawake miaka 22-35, wanaume umri wa miaka 25-35, watu wasiokua na ajira nk.
Kimsingi aina ya wateja uliowakusudia ndio inaamua aina ya maudhui ambayo utatakiwa kuandika kwenye mitandao ya kijamii.
Ifahamike matangazo ya biashara ni kwaajili ya wateja na sio kwaajili yako mwenyewe hivyo andika kulingana na aina ya wateja wako.
Kwanini Ni Muhimu Kutangaza Biashara Yako Kupitia Masoko ya Mitandao Ya Kijamii.
1.Inaongeza kufahamika kwa biashara yako.
Inasaidia biashara yako kufahamika kwa watu wengi kupitia maudhui ya picha, video na maneneo ambayo unawashirikisha watu kupitia kurasa zako.
2. Inaongeza Ushiriki wa Wateja (Improved Customer Engagement).
Mtandao unatoa fursa wateja kuwa na ushiriki mzuri katika biashara yako.
Wateja wanapata fursa ya kutoa maoni, kutuma jumbe mbalimbali jambo ambalo linawasaidia kuridhika na kujenga mahusiano imara na biashara yako.
3. Kutengeneza watembeleaje wengi.
Ni rahisi kupata idadi nzuri ya watembeleaji wa tovuli yako.
Kwa kushare link ya tovuti kwenye kurasa zako za mitandao ya kijamii jambo ambalo linaweza kuvutia na kubadili wafuasi wako kuwa wateja wako.
4.Inasaidia kuweka tovuti yako kwenye orodha ya juu katika injini ya utafutaji (Better Search Engine Ranking ).
Uzingatiaji wa kanuni za kuandika matangazo ya biashara kwenye mtandao. Inasaidia biashara kukua na kupata wateja wengine kwasababu tovuti yako ikiwa ni rahisi kufikika mtandaoni ndio namna nzuri ya kupata wateja.
Katika nyakati hizi soko la mtandaoni lina nguvu na uwezo mkubwa wa kuleta wateja katika biashara yako pamoja na kuongeza mauzo.
Washirikishe wengi maarifa haya lakini subscribe ili iwe rahisi kwako kupata new lletter.
Mwisho, matumizi ya mitandao ya kijamii inahitaji ujuzi wa namna ya kutumia ili uweze kupata kazi nyingi na zenye donge nono.
Comments
Post a Comment