Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2017

NGUVU YA FURSA KATIKA BIASHARA.

Moja kati ya eneo nyeti katika masuala ya biashara ni maamuzi yanafanyika juu ya kila fursa inayokuja. Matumizi ya fursa yanaweza kustawisha biashara yako kwa kiwango cha juu sana kuliko jinsi ambavyo unaweza kufikiri. Biashara ili iweze kuwepo lazima kuwepo na fursa ya kiabiashara, hakuna biashara kama hakuna fursa ya kibiashara hivyo kila mjasiriamali ni vema akajifunza vizuri juu ya nguvu iliyopo katika fursa. Fursa ni mazingira rafiki kwaajili ya kufanya jambo fulani. Kama mjasiriamali ni vema ukatazama kila fursa katika jicho la biashara kwasababu mtazamo wa kibiashara (business mentality)  ndiyo inayopelekea kuona fursa katika nyakati zote na katika kila hali. Aina mbalimbali ya fursa. I) Fursa ya kutumia muda. Namna unavyotumia muda wako inaweza kukusaidia kujiingizia kipato au kuongeza uwezo wako      ( increase your ability) katika masuala ya biashara. Muda unaweza kukusaidia jinsi ya kutumia rasimali watu mfano wafanyakazi wako wafanye kazi masaa mangapi ili