Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2021

MUONGOZO WA KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI

                                                                    UTANGULIZI Mfululizo wa makala hizi ni mahususi kwaajili ya kujenga uelewa utakaosaidia wajasiriamali katika kuanzisha vikundi vya ujasiriamali.  Kumekuwepo na changamoto katika kuanzisha vikundi vya ujasirimali  na hii ni kutokana na kukosa ufahamu sahihi katika namna ya kuanzisha na kuendesha shughuli za vikundi vya ujasiriamali.    Jamii inapaswa kujua umuhimu wa kufanya biashara katika mfumo wa vikundi vya ujasiriamali ili kuona hitaji la kuanzisha vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao na sio taasisi kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwasababu jamii isiposhiriki katika uanzishwaji wa kikundi kuna uwezekano mkubwa wa kikundi kuanzishwa ambacho hakina uwezo wa kusaidia wanakikundi kujenga uwezo wa  kujitegemea kiuchumi.  Moja ya sababu ambayo ilichangia taifa la Tanzania kuingia miongoni mwanchi zenye kipato cha kati ni ukuaji wa uchumi mkubwa ambao unajumuisha sekta zote za uzalishaji na wajasiriamali ni kundi