Katika kila taaluma kwenye maisha ya mwanadamu kuna taratibu zake au kuna kanuni fulani ambazo zinasaidia kutoa mwongozo kwa kila anayetaka kufanya jambo hilo ili aweze kufanya katika ubora unao kubalika. Vivyo hivyo katika biashara kuna mambo muhimu ambayo mjasiriamali anapaswa kuzingatia ili aweze kufanya kazi yake katika viwango vilivyo tukuka. Una zalisha bidhaa zako kwaajili ya nani ? hili ni swali la msingi ambalo mfanyabiashara yoyote anapaswa kujiuliza kabla ya kuanza kutengeneza bidhaa zake. Kuna utofauti mkubwa kati ya utengenezaji wa bidhaa kulingana umri, utamaduni wa watu fulani ,taaluma ya watu fulani, mila na desturi za watu fulani na wakati mwingine pia kulingana na hali ya kijiografia ya eneo husika itakuwa jambo la ajabu kama mjasiriamali ataamua kutengeneza makoti mazito na masweta wakati anategemea wateja wake wanapatikana katika ukanda wa joto. Ni vyema mfanyabiashara akajua vyema aina ya kundi katika jamii ambalo amekusudia kuliuzia baid
Jukwa maalumu kwaaji ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu biashara na ujasiriamali