Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2017

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.

Moja kati ya elimu muhimu kwa kila mtu ambaye ameamua kufanya biashara ni elimu ya USIMAMIZI WA FEDHA. Fedha inahitaji usimamizi wa hali ya juu ili iweze kuongezeka na kutimiza malengo ulionayo katika biashara yako. Unapokosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha inaweza kuzalisha matatizo kadha wa kadha katika biashara yako. Baadhi ya matatizo yanayoweza kutokea kwenye biashara yako kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri wa fedha. Unaweza kupata hasara katika biashara yako. Unaweza kupunguza kiasi cha mtaji wako. Unaweza kuingia kwenye mgogoro wa madeni. Unaweza kushindwa kununua mali ghafi kwaajili ya uzalishaji. Unaweza kupoteza thamani ya jina la biashara yako. Unaweza kupunguza thamani ya ubora wa bidhaa zako. Kuna matatizo lukuki ambayo yanaweza kujitokeza kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha hivyo elimu ya masuala ya usimamizi wa fedha ni muhimu sana katika biashara yako. Usimamizi wa fedha ni nini ? Usimamizi wa fedha ni namna ya kusim