Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2020

KUWAJALI WATEJA

Suala la huduma kwa mteja ni muhimu  katika biashara lakini kuwajali wateja ni muhimu zaidi kwasababu ni suala lenye kujenga mahusiano ya kibiashara kwa muda mrefu. Huduma kwa mteja (Customer service)  ni kitendo cha kumsaidia mteja kukamilisha muhamali fulani lakini kumjali mteja (Customer care) ni kitendo cha kumuwezesha mteja kukamilisha muhamala fulani na kumfanya mteja aweze kurudi tena kununua biadhaa au hudumu.  Je wewe ni mmoja wa watu ambao umewahi kwenda katika duka fulani ukajibiwa vibaya na muuza duka wakati ukiulizia bei ya bidhaa fulani au umewahi kufika dukani wa kwanza halafu wakaja wateja nyuma yako na wakahudumiwa wewe ukabaki, umewahi kumsalimia muuza duka na hakupokea salama yako?, umewahi kutofautiana na muuza bidhaa fulani akaanza kukutukana, kukukeji  na kukuvunjia heshima? baadhi ni mambo ambayo watu wengi wamekutana nayo wakiwa wakinunua biadhaa au huduma fulani. Maswali hayo ni vitu ambayo kwa asilimia kubwa vinafukuza mteja asiweze kurudi kununua bidhaa yako