SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Moja kati ya elimu muhimu sana kwa kila mjasiariamali ni elimu kuhusu usimamizi wa fedha, elimu ya usimamizi wa fedha ndiyo itakayo msaidia mjasiriamali kuwa na uendelevu (Stability( katika biashara yake kwasababu suala sio kuwa na biashara tu bali ni kuwa na biashara yenye kuendelea. Usimamizi wa fedha ni kitendo cha kuweka mipango na kudhibiti shughuli zote zinazo husu masuala ya fedha katika biashara, kampuni au taasisi fulani. Kwanini unapaswa kujifunza usimamizi wa fedha katika biashara yako . 1. Unapaswa kujifunza usimamizi wa fedha kwasababu ili uwezekujua ni njia ipi inaweza kukusaidia kukuza mtaji wako kama lakini katika hatua ya awali ni vema ukalifahamu hili kwasababu itakusaidia kujua mahitaji yako ya mtaji kulinga na biashara unayokusudia kuanzisha. i) Mkopo ii) Kuweka fedha zako mwenyewe iii) Mkopo na fedha zako mwenyewe 2. Unapaswa kujua usimamizi wa fedh
Jukwa maalumu kwaaji ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu biashara na ujasiriamali