Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2020

MUONGOZO WA KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASIRIMALI

  SEHEMU YA KWANZA Na; James Albert  Ni jambo la burasa kuwa na vikundi vya wajasiamali wadogowadogo kwa lengo la kuunganisha nguvu pamoja lakini pia kuweza kupata fursa mbalimbali zilizopo katika mfumo wa uchumi. Kabla ya kutoa muongozo wa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali napenda kutoa sababau za kwanini ni vizuri kuwa katika mfumo wa kikundi i)  Ili kuweza kupata msaada ya kitaalamu na kimtaji katika serikali ni lazima kuwa katika mfumo wa kikundi. ii)  Ni rahisi kupata mtaji kwasababu katika kikundi mtaji unachangiwa na wanachama wote lakini ingekuwa mtu mmoja kitendo cha kukusanya mtaji kinaweza kuchukua muda mrefu pia taasisi za kifedha kama mabenki wanatoa mikopo katika kikundi na sio mfanya biashara mdogo mojamoja kwasababu kikundi ndio kinakuwa dhamana ya mkopo.  iii) Ni rahisi kupata mafunzo kutoka katika  mashirika yasiyo ya kiseriakali na serikali kwa ujumla na rahisi serikali kuhusika na suala la kikundi kuliko mtu mojamoja. . iv) Kuna uwezekano na kuwa