Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2022

DHANA YA UONGOZI

                                                 Sehemu Ya I                        Katika mfululizo wa makala hii tutajifunza kuhusu uongozi katika maeneo yafuatayo maana ya uongozi, aina za uongozi na sifa za kiongozi hivyo karibu ufuatilie kwa kina.  Makali hizi zinaweza kukusaidia kwenye kila nyanja ya uongozi iwe na siasa, biashara au katika taasisi.  Uongozi Uongozi ni uwezo wa kuijua njia, kuipita njia na kuwa onyesha wengine njia ~ John Maxwell.  Uongozi ni uwezo au njia ya kushawishi watu ili waweze kufanya kitu au kufikia lengo fulani la kikundi kwa ridhaa yao wenyewe. Kimsingi uongozi ni dhana pana sana ambayo kila mmoja anaweza kueleza kutoka katika kona yake. Lakini kwa muktadha wa makala hii tutaangalia uongozi kutoka katika nyanja ya kuijua njia, kuipita na kuwaonyesha wengine ili waweze kuipita hiyo njia. Kiongozi anaweza kuwa wa kampuni, nchi, kikundi, taasisi fulani na jukumu la kiongozi ni kuhakikisha malengo ya taasisi, kampuni, nchi, mradi, mpango fulani yanafikiwa