Kuongeza thamani katika biashara ni kitu muhimu kwaajili ya ukuaji na mafanikio ya biashara yako kwa ujumla. Thamani katika ulimwengu wa biashara inamaanisha ubora wa bidhaa/huduma kutoka na umuhimu wake ukilinganisha na pesa anayolipia mteja. Biashara ambayo inatoa thamani kwa wateja wakati ni biashara ambayo itavutia wateja sana. Unaweza kuongeza thamani katika biashara kwa kutumia njia mbalimbali lakini wewe kama mjasiriamali unahitaji kujua ni njia ipi ni sahihi katika biashara yako. Njia za kuongeza thamani Kuwajali wateja Kuwajali wateja ni njia moja wapo ya kuongeza thamani katika biashara. Wateja wanathamani na kupenda biashara ambayo inaridhisha zaidi ya mahitaji yao. Hii inafanyika kwa kujifunza namna ya kuwajali wateja, kufanyia kazi malalamiko ya wateja, kutoa mrejesho wa wakati, kugusa hitaji la mteja wakati unamuhudumia. Mara nyingi wateja wakijaliwa vizuri huwa wanawaambia watu wengine kuhusu ubora wa huduma na bidhaa zako. jambo ambalo huongeza mauzo na mapato katika
Jukwa maalumu kwaaji ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu biashara na ujasiriamali