Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2016

Jinsi ya kupata wazo la biashara (Sehemu ya pili)

ANGALIA UNAPENDA NINI KISHA KIGEUZE KUWA  BIDHAA  AU HUDUMA. Kuna idadi kubwa ya watu ambao wamepata mawazo ya kuanzisha biashara kupitia njia hii na hatimaye kujitengenezea kipato kizuri. Kila mwanadamu kuna jambo fulani au kitu fulani ambacho yeye anapenda kufanya hivyo ni vyema ukajichunguza unapenda nini na hatimaye kugeuza hicho unachopenda kuwa bidhaa au huduma. Mfano I Kama wewe unapenda shughuli za kilimo unaweza kuanzisha shughuli za kilimo biashara (Agribusiness) ukijikita katika uzalishaji wa mazao ya biashara, pia waweza kuanzisha kiwanda cha usindikaji wa mazao ya kilimo ili kuongeza thamani na kisha kijitengenezea kipato kizuri kabisa. Mfano II Kama wewe unapenda maswala ya mitindo na urembo waweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inashughulika na utengenezaji wa nguo ,vipodozi usambazi  marashi ,mafuta ya kujipaka na bidhaa nyingine zinazohusika na mitindo na urembo.Unaweza kuanzisha saluni za kiume na za kike ilikuweza kufanya jambo unalolipenda

Jinsi ya kupata wazo la biashara (Sehemu ya kwanza).

Changamoto walionayo watu wengi sio kuanzisha biashara au kuanzisha kampuni bali ni kuanzisha biashara gani au kampuni gani,kuna watu wanafedha lakini hawajui wafanye nini na fedha hizo. Watu wengi wamekutana na changamoto  hii ya kupata wazo la biashara kiasi ambacho wamekuwa wakitamani kufanya biashara lakini hawajui ni biashara gani haswa wanapaswa kufanya. Napenda kukukaribisha kwa moyo mkunjufu katika  kusoma makala hii ambayo nitaeleza kwa uchache baadhi ya njia za kupata wazo la biashara au kuanzisha Kampuni. CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA JAMII UNAYOISHI Chunguza katika jamii unayoishi je kuna changemoto gani au zipi na je kupitia changamoto hizo unaweza kufanya biashara gani au kuanzisha kampuni gani ambayo bidhaa zake zitakuwa ni suluhu ya hiyo changamoto katika jamii husika. Njia hii mara nyingi inakupa uhakika wa soko la bidhaa zako na huduma utakayotoa kwa wananchi. Kusudi la njia hii ni kutatua changamoto inayokabili jamii husika wakati ukiendelea kujiingizia

Kongamano la uwekezaji katika kilimo

SIKU : Jumanne, May 24 saa  2:30 Asubuhi MAHALI: Julius Nyerere International Convention Centre - JNICC Shabaan Robert St/Garden Avenue, Dar es Salaam, Tanzania KUHUSU: Kusudi la kongamano hili ni kuwaweka pamoja wadau wote wa kilimo na kujadili nini kifanyike kusaidia vijana wengi kushiriki kilimo biashara Taarifa zaidi na kufanya booking ,Tembelea tovuti  ifuatayo: https://www.facebook.com/events/1555207961474847/

Umuhimu wa tovuti/mtandao kwa biashara ndogo.

Katika ulimwengu wa leo kupatikana au kutokupatika kwa biashara yako katika mtandao wa internet kutaathiri  kiasi cha mafanikio utakayopata. Ni muhimu kila mmiliki wa biashara  kuwezesha biashara yake kupatikana na kuonekana mtandaoni kwa kupitia tovuti za kompyuta,simu au kurasa za mitandao ya jamii.  Mtandao wa internet  unatakiwa uwe nguzo na nyenzo muhimu sana katika mkakati wako wa kutangaza biashara au bidhaa. Katika sehemu ya kwanza ya makala hii nitaonyesha umuhimu wa mfanyabiashara au mtu binafsi kumiliki tovuti. Tovuti nzuri ina uwezo mkubwa wa  kuipa biashara yako thamani na kukutofautisha na  washindani wenzako katika soko la bidhaa na huduma. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kumiliki tovuti na kuitumia kama chombo cha kufanya biashara na  kujitangaza. Tovuti itafanya biashara yako iaminike zaidi. Katika kizazi hiki  watu wengi zaidi hutegemea mtandao wa internet kutafuta taarifu kuhusu bidhaa au huduma flani kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Biashara yako

Ajira Yangu Business Plan Competition

“Ajira Yangu Business Plan Competition”  ni mpango mkakati wa kutatua changamoto za ajira kwa Vijana, Tanzania.  Ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana nchini, Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), kwa pamoja wamebuni mpango huu. Mpango huu  umebuniwa  kwaajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine pia. Sote tunajua kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea kama Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira, hali duni ya maisha, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mbinu jumuishi na kukosa fursa za kiuchumi. Ajira Yangu Business Plan Competition itahusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18-35, wale wanaotaka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao. Vijana hao watatakiwa kuja na mipango