UTANGULIZI Suala la malezi ni suala muhimu sana kwenye kila eneo la maisha hususani eneo la biashara ambalo makala hii imejikitaza kuelezea. Mlezi wa biashara ni mtu ambaye mjasiriamali anamchagua makusudi kwa lengo la kupata malezi katika masuala ya kibiashara. Uamuzi wa kupata mlezi wa biashara unapaswa kwa umakini mkubwa ili kuweka mazingira salama yatakayowezesha ukuaji na maendeleo ya biashara yako. Hakuna kanuni maalumu ambayo kila mfanyabiashara ameipitia ilikupata mlezi wa biashara lakini kuna dondoo muhimu ambazo ni vizuri kuzifahamu ili kuweza kupata msingi wa kufanya maamuzi yenye tija. Kwanini unahitaji kuwa na mlezi katika biashara? i) Kuepuka makosa ambayo yanaweza kuepukika ii) Kuwa na mshauri na mwangalizi iii) Kuongeza kiwango cha uwajikabaji iv) Kuongeza mtandao wa kibiashara v) Kuwa na mtu wa kumueleza changamoto ili kupunguza msongo wa mawazo Kama mfanya biashara na mjasiriamali ni vizuri ukawa na mlezi w
Jukwa maalumu kwaaji ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu biashara na ujasiriamali