Skip to main content

KUWAJALI WATEJA





Suala la huduma kwa mteja ni muhimu  katika biashara lakini kuwajali wateja ni muhimu zaidi kwasababu ni suala lenye kujenga mahusiano ya kibiashara kwa muda mrefu. Huduma kwa mteja (Customer service)  ni kitendo cha kumsaidia mteja kukamilisha muhamali fulani lakini kumjali mteja (Customer care) ni kitendo cha kumuwezesha mteja kukamilisha muhamala fulani na kumfanya mteja aweze kurudi tena kununua biadhaa au hudumu. 

Je wewe ni mmoja wa watu ambao umewahi kwenda katika duka fulani ukajibiwa vibaya na muuza duka wakati ukiulizia bei ya bidhaa fulani au umewahi kufika dukani wa kwanza halafu wakaja wateja nyuma yako na wakahudumiwa wewe ukabaki, umewahi kumsalimia muuza duka na hakupokea salama yako?, umewahi kutofautiana na muuza bidhaa fulani akaanza kukutukana, kukukeji  na kukuvunjia heshima? baadhi ni mambo ambayo watu wengi wamekutana nayo wakiwa wakinunua biadhaa au huduma fulani. Maswali hayo ni vitu ambayo kwa asilimia kubwa vinafukuza mteja asiweze kurudi kununua bidhaa yako na anapozungumza na watu wengine huwa anawashawishi wasije kununua hizo huduma kwako. 

Tafiti zinaonyeshaa asilimia kuwa ya wateja wapya wa benki ni wateja ambao walishawishiwa kujiunga na huduma za kibenki kupitia ndugu na  marafiki zao. Hii inamaana walipata huduma bora kwa kiasi cha kuweza kuwapendekeza (recommend) benki kwa marafiki zao lakini kama wasingepata huduma bora wasingeweza kuwashawishi marafiki zao. 

Kama mjasiriamali ni vema ukafiri kujenga mahusiano ya kibiashara yatakayo dumu kwa muda mrefu kwa kila mteja unayepata fursa ya kukutana naye. Kujali mteja ni ujuzi unaoweza kujengwa ndani ya mtu ili aweze kufanya vizuri katika biashara aliyopo. Kuna makapuni mengi ambayo yamewekeza fedha nyingi katika mafunzo ya kumjali mteja kwa wafanyakazi wake ambao wanakutana na wateja katika shughuli za kila siku. 




Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z