MUONGOZO WA KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI

 

                                                                 UTANGULIZI










Mfululizo wa makala hizi ni mahususi kwaajili ya kujenga uelewa utakaosaidia wajasiriamali katika kuanzisha vikundi vya ujasiriamali. 

Kumekuwepo na changamoto katika kuanzisha vikundi vya ujasirimali  na hii ni kutokana na kukosa ufahamu sahihi katika namna ya kuanzisha na kuendesha shughuli za vikundi vya ujasiriamali.  

Jamii inapaswa kujua umuhimu wa kufanya biashara katika mfumo wa vikundi vya ujasiriamali ili kuona hitaji la kuanzisha vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao na sio taasisi kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwasababu jamii isiposhiriki katika uanzishwaji wa kikundi kuna uwezekano mkubwa wa kikundi kuanzishwa ambacho hakina uwezo wa kusaidia wanakikundi kujenga uwezo wa  kujitegemea kiuchumi. 


Moja ya sababu ambayo ilichangia taifa la Tanzania kuingia miongoni mwanchi zenye kipato cha kati ni ukuaji wa uchumi mkubwa ambao unajumuisha sekta zote za uzalishaji na wajasiriamali ni kundi muhimu sana kama sehemu ya uzalishaji hivyo ubora wa vikundi vya ujasirimali vinamchango chanya katika maendeleo na ukuaji wa uchumi. Faida ambazo tunaweza kuzipata kwa kuwa na vikundi bora vya ujasiriamali. 

i) Upatikanaji wa ajira
ii) Chanzo cha kipato kupitia kodi na tozo mbalimbali mfano ushuru na zinginenezo
iii) Upatikanaji wa dhamana katika taasisi za kifedha
iv) Ongezeko la mtaji kwa wajasiriamali

Itaendelea 


Imeandaliwa na James Albert 
Simu 0717162510
Barua pepe jamesalbert157@gmai.com






















Comments

Popular posts from this blog

Namna Ya Kuanzisha Biashara

Biashara Ya Mbao.

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO.