Sehemu Ya I
Katika mfululizo wa makala hii tutajifunza kuhusu uongozi katika maeneo yafuatayo maana ya uongozi, aina za uongozi na sifa za kiongozi hivyo karibu ufuatilie kwa kina.
Makali hizi zinaweza kukusaidia kwenye kila nyanja ya uongozi iwe na siasa, biashara au katika taasisi.
Uongozi
Uongozi ni uwezo wa kuijua njia, kuipita njia na kuwa onyesha wengine njia ~ John Maxwell.
Uongozi ni uwezo au njia ya kushawishi watu ili waweze kufanya kitu au kufikia lengo fulani la kikundi kwa ridhaa yao wenyewe.
Kimsingi uongozi ni dhana pana sana ambayo kila mmoja anaweza kueleza kutoka katika kona yake.
Lakini kwa muktadha wa makala hii tutaangalia uongozi kutoka katika nyanja ya kuijua njia, kuipita na kuwaonyesha wengine ili waweze kuipita hiyo njia.
Kiongozi anaweza kuwa wa kampuni, nchi, kikundi, taasisi fulani na jukumu la kiongozi ni kuhakikisha malengo ya taasisi, kampuni, nchi, mradi, mpango fulani yanafikiwa.
Kuna ombwe (gap) kubwa kati ya hali ya sasa ya taasisi ambayo kiongozi anatakiwa kuongeza na ile hali inayotamaniwa hapo baadae (desired future).
Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wengien kufika katika hali ambayo taasisi inatarajia katika wakati ujao.
Kuna aina 3 za Uongozi
i. Uongozi wa ki-imla (Autocratic leadership)
ii. Uongozi wa Kidemokrasia ( Democratic Leadership)
iii. Uongozi wa kirasimu (Beaurocratic Leadership )
Uongozi wa ki-imla (Autocratic leadership)
Hii ni aina ya uongozi ambao haujali maoni ya watu wengine yaani kila anachowazo kiongozi ndio kitakachofanyika haijalishi athari zake.
Hii ni aina ya uongozi ambayo huleta maumivu makali sana katika maisha ya watu wengine kwasababu haujali hisia za watu wengine katika utendaji wa kila siku.
Itaendelea sehemu I
Comments
Post a Comment