Skip to main content

Hatua tisa za kuanzisha biashara.




Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu.

Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria.

Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi:


  1. Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan)

Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi.


  1. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara


Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini.


  1. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako.


Tafuta ushauri wa namna ya kuchagua eneo ambalo ni rafiki kwa  aina ya biashara unayotaka kufungua na pia ni rafiki kwa wateja watarajiwa. Pia fanya utafiti ili kuweza kuchagua eneo sahihi la biashara yako.


  1. Tafuta mtaji kwa ajili ya biashara yako


Tafuta mikopo yenye riba nafuu na yenye masharti ambayo  utayamudu  huku ukizingatia hali yako ya kiuchumi (Usijiingize kwenye mkopo wowote ambao hujui namna ambavyo utaweza kuulipa). Njia mbadala ya kupata mtaji ni kujiunga na kuchangia nguvu na wajasiriamali wenzako au kujiunga na mtu au taasisi yenye fedha ambazo ipo na utayari wa kuziwekeza kwenye biashara/mradi (venture capital). Usisahau mtaji wa kwanza ni wazo la biashara ulilonalo lakini pia kuna aina ya biashara ambazo hauhitaji mtaji kwa maana ya fedha mfano biashara ya kuandaa na kusimamia matukio ( Event Planning and Management).


  1. Amua mfumo  wa kisheria wa  umiliki ambao  utakaifaa biashara yako


Amua aina ya umiliki ambao ni mwafaka zaidi kwa ajili ya biashara yako: Umiliki binafsi(sole proprietorship), biashara ya ushirikiano(partnership), kampuni(corporation)  au chama cha ushirika(cooperative).


  1. Sajili jina la biashara yako.


Sajili jina la biashara yako katika mamlaka ya usajili wa biashara katika nchi yako ( kwa Tanzania mamlaka husika ni BRELA). Kitendo cha kusajili jina la biashara yako kitaipa biashara mtazamo chanya ( credibility) kwenye macho ya jamii na wateja watarajiwa.


  1. Jisajili kwenye mamlaka za kodi na pia jisajili kwenye mamlaka za za mji au jiji ili kupata vibali vya kufanya biashara katika eneo husika.


  1. Jifunze  haki na wajibu  wa mwajiri na mwajiriwa.


Katika uhai wa biashara yako utahitaji kuajiri wasaidizi na ili kukwepa kufikishwa katika vyombo vya sheria ni vyema ukajifunza haki zako(mwajiri) na haki za mwajiri kwa mujibu wa sheria za nchi mapema ili wakati utakapo fika uweze kuzitimiza kikamilifu.


Mfululizo wa makala zinazochambua kila hatua kwa kina zitafuata hivi karibuni.

WITO


Kama umependezwa na makala hii tafadhali washirikishe wenzako kwenye mitandao ya jamii ili na wao wapata fursa ya kujifunza.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z