Skip to main content

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa




Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu.

Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso.

Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online).

Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri.Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya.

1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa zako ilikujua ni bidhaa gani inayohitajika sokoni ?.Utafiti ndio utakao kupa jawabu la aina ya bidhaa ambayo inahitajika sokoni hivyo kama mjasiriamali usikurupuke tuu bila kuwa na uhakika wa aina ya bidhaa au huduma ambayo inahitajika sokoni.

2.Je soko la bidhaa yako ni wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi pia itakusaidia ufahamu gharama ya kufika sokoni kama utaamua kuuzia sokoni ,kama bidhaa yako itakuwa inauzika katika eneo la uzalishaji inamaana swala la gharama za usafirishaji utaliepeuka lakini kwa  mjasiriamali ambaye hazalishi bidhaa kwake swala la gharama ya usafiri wa kupeleka bidhaa yake sokoni ni muhimu sana kulifahamu.Mfano kama unanunua alizeti Singida ni vizuri kujua gharama ya usafiri kutoka Singida kwenda kwenye soko husika la hiyo bidhaa.

3.Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni ni vizuri kufahamu mambo hayo mawili muhimu ilikuepeka na uzalishaji mwingi ambao utapelekea kushusha bei ya bidha yako na kupunguza faida pili ni kuzalisha bidhaa yako sawasawa na majira ya soko mfano huwezi kuuza masweta na makoti wakati wa joto hivyo itakulazimu kusubiri nyakati za baridi kwasababu mzunguko wa bidhaa hizo huwa ni mkubwa wakati huo.

4.Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi,siku zote mfanya biashara huwa anazalisha bidhaa zenye kukidhi matakwa ya mteja sokoni hivyo ni vizuri kufahamu wateja wako ni kina nani na je wanahitaji bidhaa zenye ubora gani ? .Mfano kama wateja wako ni wanawake ni lazima bidhaa yako iendane na mahitaji yao kwa wakati huo (fashion).

5.Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo wakutosheleza mahitaji yao wewe pekee yako .Kama huwezi kukidhi kiwango ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza uzalishaji au kwa kuungana na wazalishaji wengine.


6.Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo na faida zaidi kwako baada ya kuondoa gharama ya kupeleka bidhaa zako sokoni ) Ila ukiamua kuuzia sokoni hakikisha unakuwa na  uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko sokoni katika ubora wa bidhaa na wakati mwingine ushindani katika bei ya bidhaa .

Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes