Skip to main content

Piga hatua katika biashara yako



Hatua ni umbali kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine au kutoka kiwango kimoja kwenda kiwango kingine. Mtu ambaye hapigi hatua katika biashara yake ni mtu ambaye yuko kwenye kiwango kimoja tu cha biashara kwa kipindi cha muda mrefu.

Mtu anapokuwa anapanda ngazi au kushuka ni lazima apige hatua moja ikifuatiwa na hatua nyingine na kadri atakavyokuwa akiendelea ndivyo atakuwa akiikaribia hatima yake au mahali alipotakiwa kufika. Hatua kwenye biashara ni mfano wa ngazi hivyo unapaswa kupiga hatua moja kwenda nyingine ili uweze kufikia hatima yako.

Katika biashara kuna watu aina tatu.

(i) Watu ambao hupiga hatua kwenda mbele mfano mwaka jana alikuwa na mtaji wenye thamani ya shilling 1,000,000 mwaka huu ameongeza mtaji wake kufikia thamani ya shilingi 1,500,000.

(ii) Watu ambao hawapigi hatua kabisa mfano mwaka jana alikuwa na mtaji wenye thamani ya 500,000 na mwaka huu thamani ya mtaji wake ni shilingi 500,000.

(iii) Watu ambao wanapiga hatua kurudi nyuma mfano mwaka jana alikuwa na mtaji wa shilingi 1,000,000 lakini mwaka huu mtaji wake umepungua thamani kufikia shilingi 700,000.

Kila kitu katika maisha kina hatua ambazo kinapaswa kupitia ilikufikia katika utimilifu wake hata mwadanamu kuna hatua mbalimbali za ukuaji ambazo anapaswa kupitia kutoka utoto mpaka utuzima. Mtoto anapokaa kwenye hatua moja ya ukuaji kwa kipindi kirefu huwa tunasema mtoto huyo amedumaa, biashara inapokaa katika hatua moja kwa kipindi kirefu biashara hiyo husemekana ya kuwa imedumaa au haiendelei, mti wa matunda unapokaa muda mrefu bila kuzaa huwa tunasema mti huo umedumaa.

Kama unahitaji kuwa na uwekezaji au biashara yenye tija ni vema suala la kupiga hatua ukalipa thamani kubwa kwasababu ndio linakueleza kama biashara yako inakuwa au la. Thamani ya mtaji wako iko ndani ya muda hivyo endapo hautajifunza kufanya vitu ambavyo vitakusaidia kupiga hatua huenda baada ya muda ukiangalia thamani ya mtaji wako utakuta umeshuka thamani kwa kiwango kikubwa. 

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kupelekea  biashara yako kutopiga hatua stahiki mfano kutokuwa na mpango kazi katika biashara , kukosa vipaumbele katika biashara yako, kutopenda kujifunza mambo mapya ambaye yataongeza thamani katika biashara yako , kutofanya tathimini ya biashara yako, Kuwa na mipango mizuri isiyokuwa na utekelezaji na kuzikimbia changamoto badala ya kuzikabili. Jambo baya unapokimbia changamoto ni kwamba hautajifunza nini chakufanya na pia kuna uwezekano wa changamoto hiyohiyo kujirudia lakini unapokabiliana na changamoto itakusaidia nini chakufanya na kuweka mpango mkakati wa kukabiliana nayo mapema ( proactive strategy).

Ni muhimu sana kupiga hatua katika biashara yako  ili kuweza kufikia hatima yako na kuwa mtu mwenye furaha. Fanya tathimini ya kina katika biashara yako ili kujua kama unapiga hatua au la na kisha weka mpango mkakati wa kuhakikisha unapiga hatua vema ili kufikia hatima yako.

Imeandaliwa na 
James Albert
Namba ya simu 0717161210& 0756471244
Baraua pepe jamesalbert157@gmail.com
2016 

Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z