Katika kila taaluma kwenye maisha ya mwanadamu kuna taratibu zake au kuna kanuni fulani ambazo zinasaidia kutoa mwongozo kwa kila anayetaka kufanya jambo hilo ili aweze kufanya katika ubora unao kubalika.
Vivyo hivyo katika biashara kuna mambo muhimu ambayo mjasiriamali anapaswa kuzingatia ili aweze kufanya kazi yake katika viwango vilivyo tukuka.
Una zalisha bidhaa zako kwaajili ya nani ? hili ni swali la msingi ambalo mfanyabiashara yoyote anapaswa kujiuliza kabla ya kuanza kutengeneza bidhaa zake. Kuna utofauti mkubwa kati ya utengenezaji wa bidhaa kulingana umri, utamaduni wa watu fulani ,taaluma ya watu fulani, mila na desturi za watu fulani na wakati mwingine pia kulingana na hali ya kijiografia ya eneo husika itakuwa jambo la ajabu kama mjasiriamali ataamua kutengeneza makoti mazito na masweta wakati anategemea wateja wake wanapatikana katika ukanda wa joto. Ni vyema mfanyabiashara akajua vyema aina ya kundi katika jamii ambalo amekusudia kuliuzia baidhaa zake.
Je upatikanaji wa mali ghafi ukoje ? mali ghafi ni vitu vyote ambavyo vinasaidia katika utengenezaji wa bidhaa, mfano kama wewe una mghahawa basi mali ghafi yako ni chumvi, sukari, mchele nk. Kujua upatikanaji wa mali ghafi kutakusaidia kujua ni wapi ufungue kituo chako cha biashara, itakusaidia kujua upange bei gani kulingana na gharama ya upatikanaji wa mali ghafi.
Je bidhaa yako ni ya msimu au la ? kila mfanyabishara anapaswa kujua aina ya bidhaa anayozalisha je inasoko la kudumu au ni bidhaa ya msimu tu. Kupitia kujua aina ya soko la bidhaa zake itamsaidia kujua ni kiwango gani anapaswa kuzalisha au kununua na kisha kwenda kuuza kwenye soko husika.
Je washindani wako ni kina nani ? washindani wako ni makampuni au watu wanaozalisha bidhaa zinazofanana na za kwako. Ukijua washindani wako itakusaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora na utofauti ukilinganisha na wao hivyo utakuwa na uhakika wa soko la bidhaa zako.
Je utahitaji kufanya matangazo ya biashara yako ? Ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa kidigitali, na kumekuwa na matumizi makubwa ya teknolojia ya habari na wasaliliano hivyo ni vyema ukajua njia sahihi ya kutangaza biashara yako. Kuna utofauti mkubwa wa kutangaza biashara kwenye redio, televisheni, majarida, vipeperushi, mabango na hata katika tovuti. Mfano, matangazo ya kwenye mitandao ya kijamii yanapaswa kuwa na ujumbe wa moja kwa moja na mvuto wa picha wa hali ya juu kiasi kwamba tangazo hilo litakamata akili ya anayeperuzi kwa urahisi ili aendelee kusoma na kuliangalia tangazo hilo.
Uzuri wa kazi yoyote katika biashara unategemea na umakini wa mfanyabishara katika kuzingatia mambo muhimu yenye kutoa mwongozo wa kibiashara. Ni hekima kwa mfanyabiashara kujifunza mambo hayo muhimu kabla ya kuingia katika biashara. Swala la msingi zaidi analopaswa kufahamu mfanyabiashara ni kwamba kuna mambo mengi katika biashara hivyo anaweza kujifunza moja baada ya jingine huku akiweka katika matendo kile anachojifunza. Mfano anaweza kujifunza maswala ya Soko, Usimamizi wa biashara, Usimamizi wa miradi nk.
Itaendelea.
By
Itaendelea.
By
James Albert.
Comments
Post a Comment