Skip to main content

USIMAMIZI WA FEDHA KATIKA BIASHARA YAKO

                                               SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI 




Moja kati ya elimu muhimu sana kwa kila mjasiariamali ni elimu kuhusu usimamizi wa fedha, elimu ya usimamizi wa fedha ndiyo itakayo msaidia mjasiriamali kuwa na uendelevu  (Stability( katika biashara yake kwasababu suala sio kuwa na biashara tu bali ni kuwa na biashara yenye kuendelea.

Usimamizi wa fedha ni kitendo cha kuweka mipango na kudhibiti shughuli zote zinazo husu masuala ya fedha katika biashara, kampuni au taasisi fulani. 

Kwanini unapaswa kujifunza usimamizi wa fedha katika biashara yako .

1. Unapaswa kujifunza usimamizi wa fedha kwasababu ili uwezekujua ni njia ipi inaweza kukusaidia kukuza mtaji wako kama lakini katika hatua ya awali ni vema ukalifahamu hili kwasababu itakusaidia kujua mahitaji yako ya mtaji kulinga na biashara unayokusudia kuanzisha.  

i) Mkopo 
ii) Kuweka fedha zako mwenyewe
iii) Mkopo na fedha zako mwenyewe

2. Unapaswa kujua usimamizi wa fedha kwasababu itakusaidi kuweka usalama katika biashara yako, mjasirimali yoyote yule mwenye elimu ya masuala ya fedha kuwekeza kwenye sehemu salama ya fedha zake yaani kwa ufupi mahali ambapo fedha zake zitaendelea kujizalisha na sio kupotea. 

Itaendelea

Imeandaliwa na

James Albert

Nambari ya simu +255717 162 510
Barua pepe jamesalbert157@gmail.com

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z