MALEZI YA BIASHARA

                                                       UTANGULIZI



Suala la malezi ni suala muhimu sana kwenye kila eneo la maisha hususani eneo la biashara ambalo makala hii imejikitaza kuelezea. 

Mlezi wa biashara ni mtu ambaye mjasiriamali anamchagua makusudi kwa lengo la kupata malezi katika masuala ya kibiashara. 

Uamuzi wa kupata mlezi wa biashara unapaswa kwa umakini mkubwa ili kuweka mazingira salama  yatakayowezesha ukuaji na maendeleo ya biashara yako. 

Hakuna kanuni maalumu ambayo kila mfanyabiashara ameipitia ilikupata mlezi wa biashara lakini kuna dondoo muhimu ambazo ni vizuri kuzifahamu ili kuweza kupata msingi wa kufanya maamuzi yenye tija. 

Kwanini unahitaji kuwa na mlezi katika biashara?

i) Kuepuka makosa ambayo yanaweza kuepukika

ii) Kuwa na mshauri na mwangalizi

iii) Kuongeza kiwango cha uwajikabaji

iv) Kuongeza mtandao wa kibiashara

v) Kuwa na mtu wa kumueleza changamoto ili kupunguza msongo wa mawazo 

Kama mfanya biashara na mjasiriamali ni vizuri ukawa na mlezi wako katika masuala ya biashara yako. 

Zifuatazo ni dondoo muhimu katika kufanya maamuzi wa mlezi wa biashara 

i) Mwenye maono

ii) Mwenye uzoefu katika biashara

iii) Mwenye uongozi bora katika biashara yake

iv) Mwenye mtazamo chanya na imani na wewe

 


Imeandaliwa na James Albert 

Namba ya whatsapp 0717162510

Barua pepe jamesalbert157@gmail.com


Comments

Popular Posts