Namna ya utengeneza chapa ya biashara yako ni muhimu sana ili uweze kuliteka soko la bidhaa/huduma unayoiuza.
Ni mchakato wa kutengeneza utambulisho wa pekee ili kijitofautisha wa washindani wako sokoni.
Chapa (brand) nzuri inavutia wateja wako na kuwasaidia kuweza kukuamini katika biashara yako
kujenga chapa (brand) sio jambo jepesi lakini ni kitu ambacho kinawezakana na ni muhimu kwaajili ya mafanikio ya muda mrefu katika biashara yako.
Biashara ambayo imejengewa brand nzuri ina vutia wateja wengi na ambao ni sahihi kwaajili ya biashara.
Ili kujenga brand inahitaji kujua aina ya wateja ambao unawakusudia, kujua mahitaji yao na vitu wanavyopendelea.
Katika makala hii tutajifunza namna ya kutengeneza brand ya biashara yako.
Haijalishi wewe ni mtu mwenye biashara mpya sokoni au umekuwepo sokoni kwa muda mrefu lakini ukweli ni kwamba kutengeneza brand ya pekee ni suala muhimu.
Namna ya kutengeneza brand.
i. Kabla ya kuanza kubrand biashara yako ni muhimu kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na biashara yako, kujua mambo yote ya msingi kuhusu biashara yako.
Unahitaji kubaini maono ya biashara yako, misheni ya biashara yako na vitu gani unazongatia katika kuuza huduma/bidhaa.
Uelewa wa kutosha kuhusu biashara yako itakusaidia brand iweze kuakisi biashara yako na wateja wako kuwa na sauti katika akili yao kahusu biashara yako.
Bainisha maono yako na misheni yako
Misheni yako lazima ibainishe baishara yako inafanya nini, inamuhudumia nani na upekee wake katika soko.
Maono yako lazima yaonyeshe picha kubwa ya baadae katika biashara yako
Bainisha vitu unavyozingatia katika biashara yako.
Vitu hivyo ni kanunu zinazokuongoza na kubaini utamaduni wa biashara yako.
Mfano wa vitu hivyo ni kama utu, uwazi, uwajibikaji, timu na mambo mengi ambayo yanatengeneza kanunu katika kutoa huduma.
Kimsingi vitu ambayo unazingatia katika kutoa huduma (Core Values) vitatakiwa kuakisi branda ya biashara yako.
Mwisho, chapa nzuri ya biashara inaleta utambulisho wa pekee sokoni na kuvutia wateja ambao umewakusudia.
Comments
Post a Comment