Skip to main content

Masoko Ya Mitandao Ya Kijamii.

 Masoko ya mitandao ya kijamii ni mchakato wa kutengeneza na kushirikisha maudhui  watu yenye lengo la kutangaza huduma/bidhaa yako kupitia mitandao ya kijamii.

Baadhi ya mitandao ya kijamii ni kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Threads na Truth Socia Media.

Lengo la masoko ya mitandao ya kijamii ni kuwajengea wateja uelewa.

Kuhusu huduma/bidhaa zako, kuongeza watembeleaji wa tovuti ya biashara na kuongeza mauzo kwa ujumla.

Masoko ya mitandao ya kijamii yanahitaji ufahamu wa hali ya juu kufikia wateja ambao umewakusudia.

Mfano wateja kusudiwa wanaweza kuwa wanawake miaka 22-35, wanaume umri wa miaka 25-35, watu wasiokua na ajira nk.

Kimsingi aina ya wateja uliowakusudia ndio inaamua aina ya maudhui ambayo utatakiwa kuandika kwenye mitandao ya kijamii.

Ifahamike matangazo ya biashara ni kwaajili ya wateja na sio kwaajili yako mwenyewe hivyo andika kulingana na aina ya wateja wako.

Kwanini Ni Muhimu Kutangaza Biashara Yako Kupitia Masoko ya Mitandao Ya Kijamii. 

1.Inaongeza kufahamika kwa biashara yako.

Inasaidia biashara yako kufahamika kwa watu wengi kupitia maudhui ya picha, video na maneneo ambayo unawashirikisha watu kupitia kurasa zako.

2. Inaongeza Ushiriki wa Wateja (Improved Customer Engagement).

Mtandao unatoa fursa wateja kuwa na ushiriki mzuri katika biashara yako.

Wateja wanapata fursa ya kutoa maoni, kutuma jumbe mbalimbali jambo ambalo linawasaidia kuridhika na kujenga mahusiano imara na biashara yako.

3. Kutengeneza watembeleaje wengi.

Ni rahisi kupata idadi nzuri ya watembeleaji wa tovuli yako.

Kwa kushare link ya tovuti  kwenye kurasa zako za mitandao ya kijamii jambo ambalo linaweza kuvutia na kubadili wafuasi wako kuwa wateja wako.

4.Inasaidia kuweka tovuti yako kwenye orodha ya juu katika injini ya utafutaji (Better Search Engine Ranking ).

Uzingatiaji wa kanuni za kuandika matangazo ya biashara kwenye mtandao.  Inasaidia biashara kukua na kupata wateja wengine kwasababu tovuti yako ikiwa ni rahisi kufikika mtandaoni ndio namna nzuri ya kupata wateja.

Katika nyakati hizi soko la mtandaoni lina nguvu na uwezo mkubwa wa kuleta wateja katika biashara yako pamoja na kuongeza mauzo.

Washirikishe wengi maarifa haya lakini subscribe ili iwe rahisi kwako kupata new lletter.

Mwisho, matumizi ya mitandao ya kijamii inahitaji ujuzi wa namna ya kutumia  ili uweze kupata kazi nyingi na zenye donge nono.

Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z