Skip to main content

Kupata Wazo la Biashara.

 Kupata wazo la biashara ni changamoto inayowakabili watu wengi katika maisha yao. 

Baadhi ya watu wanatamani kufanya biashara lakini hawajui ni biashara gani wafanye. 

Katika makala hii nitaeleza baadhi ya mbinu/njia ambazo unaweza kutumia kupata wazo la biashara. 

Ni ukweli uliodhahiri kabla ya jambo lolote kufanyika huwa linaanzia katika wazo (idea).

Wazo ni asili ya mambo yote yanayofanyika katika maisha yetu ya kila siku.

Ujenzi wa nyumba ulianzia katika wazo.

Ugunduzi wa jambo lolote huanzia katika wazo.

Utengenezaji wa kifaa chochote ulianzia katika wazo.

Mahusiano huanzia katika wazo.

Kimsingi biashara yoyote unayoiona ilianzia katika wazo (idea) ambalo alikua nalo mtu fulani.

Namna wafanya biashara walivyopata wazo la biashara ni tofauti kutoka mmoja kwingine mwingine. 

Inahitaji kuwa na mtazo huru tena wa kibiashara ili uwezo kupata wazo la biashara ambalo utalifanyia kazi. 

Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kukusaidia  kupata wazo la biashara

1. KIPAJI

Kipaji ni uwezo wa asili ambao mtu anazaliwa nao unaomsaidia kufanya kazi zenye ubora wa hali ya juu.

Uwezo huu ni maalumu katika utendaji wa jambo fulani

Kuna mtu anauwezo mkubwa wa kuandika, kuimba, kushauri, kuongea na halaiki ya watu, kupamba, kupika, kuongoza watu na kadhalika. 

Kila uwezo wa asili ambao mtu amepewa unaweza kutumika kupata wazo la biashara na kuingiza kipata. 

Watu wengine unaowaona katika ulimwengu wa biashara kipaji kinatumika kwa kiwango kikubwa sana. 

Kipaji anazaliwa nacho mtu lakini kinaweza kuendelezwa ili kuongeza ufanisi.

Kila uwezo ambao Mungu amempa mtu unatoa fursa ya kujitengenezea kipato na kuboresha maisha yake.

Kupitia kipaji unaweza kupata wazo la biashara mfano kama wewe ni mchoraji unaweza kuangalia katika zama hizi ni uchoraji wa aina gani unahitajika .

Je ni uchoraji wa picha za watu

Uchoraji wa mabango

Je ni uchoraji wa nyumba

Je ni uchoraji wa vitu vya asili. 

Mwisho, uwezo wako wa asili ni nyenzo bora katika kupata wazo la biashara ambayo utaifanya vizuri na kwa ubora wa hali ya juu. 

Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z