Skip to main content

Jinsi ya kupata wazo la biashara (Sehemu ya pili)





ANGALIA UNAPENDA NINI KISHA KIGEUZE KUWA  BIDHAA  AU HUDUMA.

Kuna idadi kubwa ya watu ambao wamepata mawazo ya kuanzisha biashara kupitia njia hii na hatimaye kujitengenezea kipato kizuri. Kila mwanadamu kuna jambo fulani au kitu fulani ambacho yeye anapenda kufanya hivyo ni vyema ukajichunguza unapenda nini na hatimaye kugeuza hicho unachopenda kuwa bidhaa au huduma.

Mfano I
Kama wewe unapenda shughuli za kilimo unaweza kuanzisha shughuli za kilimo biashara (Agribusiness) ukijikita katika uzalishaji wa mazao ya biashara, pia waweza kuanzisha kiwanda cha usindikaji wa mazao ya kilimo ili kuongeza thamani na kisha kijitengenezea kipato kizuri kabisa.

Mfano II
Kama wewe unapenda maswala ya mitindo na urembo waweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inashughulika na utengenezaji wa nguo ,vipodozi usambazi  marashi ,mafuta ya kujipaka na bidhaa nyingine zinazohusika na mitindo na urembo.Unaweza kuanzisha saluni za kiume na za kike ilikuweza kufanya jambo unalolipenda na pia kujitengenezea kipato.

Mfano III
Kama wewe unapenda kusafiri unaweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inatoa huduma za usafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine wakati ukijipanga kutanua wigo mpaka kutoa huduma za usafiri kimataifa.Waweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inatoa huduma za usafiri katika sherehe mbalimbali kama harusi au kuingia mikataba na taasisi ambazo hazina magari ya kutosha hivyo kutoa huduma hiyo kwao na wakati ukijiingizia kipato.

Mfano IV
Kama unapenda tasnia ya teknolojia ya habari hii inaweza kuwa njia nzuri ya kuanzisha kampuni ambayo itajikita katika uandaji wa vipindi vya redio na televisheni pia unaweza kuanzisha kituo cha kurusha matangazo kwa njia ya redio au televisheni.Unaweza kuanzisha studio ya kurekodia matangazo ya biashara na kisha kuingia mikataba na makapuni au taasisi ambazo utakuwa unawaandalia matangazo yao ya biashara,pia unaweza kuanzisha huduma ya uandaaji wa makala mbalimbali wakati unafurahia kufanya unachopenda pia utakuwa unajitengeneza kipato kizuri .

Mfano V
Kama wewe unapenda maswala ya ufugaji kama kuku,ng'ombe ,mbuzi ,njiwa ,ufugaji wa samaki unaweza kuanzisha ufagaji biashara. Kwa hiyo utafuga mifugo kwasababu unapenda kufuga na wakati huohuo utakuwa unajitengenezea kipato .

Mfano VI
Kama wewe unapenda maswala ya uandishi na usomaji wa vitabu ,majarida unaweza kuanzisha kampuni ya kuchapisha (Publication Company)ambayo itajikita katika uchapishaji wa  vitabu,majarida ,tisheti na vipeperushi hivyo kujitengenezea kipato.

Faida za njia hii

Tafiti zinaonyesha watu wengi wanaofanya kazi wanazozipenda huwa wanafanya kazi katika ufanisi wa hali ya juu.Mtu ambaye anafanya kazi anayoipenda ni mtu ambaye huwa na furaha maisha mwake, pia utakuwa unajitengenezea kipato kizuri hivyo utakapo amua kutumia njia hii kupata wazo la biashara utapata faida hizo nilizozitaja hapo juu.

Changamoto na suluhu yake.

Ushindani ndio changamoto kubwa katika njia hii hivyo unahitaji kuja na ubunifu wa hali ya juu ilikutoa huduma nzuri kulingana na ushindani ulioko sokoni; kwasababu unaweza kuta kitu unachopenda kuna mtu mwingine anakipenda pia na tayari ameshaanza kutoa huduma au bidhaa hiyo sokoni. Ukitaka kufanikiwa katika njia hii unatakiwa kutoa bidhaa nzuri na zatofauti na yule mshindani wako ilikuweza kupata wateja wakutosha.

Ushauri 

Kabla ya kuanzisha biashara husika kupitia njia hii ni vema ukafanya tafiti za kutosha kuhusu soko la hiyo biashara unayotakakufanya na kisha kujua kama unachopenda kina weza kuwa bidhaa au huduma inayohitajika sokoni.Nakushauri ndugu yangu usikimbilie kuanzisha biashara bila kuwa na taarifa sahihi juu ya soko husika kwasababu mfanyabiashara  huzalisha bidhaa zake  kwaajili ya kuuza sokoni na si vinginevyo.

Itaendelea sehemu ya III

Imeandaliwa na James Albert. 
Namba ya simu +255717162510
Barua pepe jamesalbert157@gmail.com 







Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z