Skip to main content

Jinsi ya kupata wazo la biashara (Sehemu ya kwanza).


Changamoto walionayo watu wengi sio kuanzisha biashara au kuanzisha kampuni bali ni kuanzisha biashara gani au kampuni gani,kuna watu wanafedha lakini hawajui wafanye nini na fedha hizo. Watu wengi wamekutana na changamoto  hii ya kupata wazo la biashara kiasi ambacho wamekuwa wakitamani kufanya biashara lakini hawajui ni biashara gani haswa wanapaswa kufanya.

Napenda kukukaribisha kwa moyo mkunjufu katika  kusoma makala hii ambayo nitaeleza kwa uchache baadhi ya njia za kupata wazo la biashara au kuanzisha Kampuni.

CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA JAMII UNAYOISHI

Chunguza katika jamii unayoishi je kuna changemoto gani au zipi na je kupitia changamoto hizo unaweza kufanya biashara gani au kuanzisha kampuni gani ambayo bidhaa zake zitakuwa ni suluhu ya hiyo changamoto katika jamii husika. Njia hii mara nyingi inakupa uhakika wa soko la bidhaa zako na huduma utakayotoa kwa wananchi. Kusudi la njia hii ni kutatua changamoto inayokabili jamii husika wakati ukiendelea kujiingizia kipato.

Mfano  I:- Katika kijiji cha WATANZANIA TUMEAMUA kuna changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama hivyo unaweza kuchimba kisima na kuanzisha biashara ya kuuza maji kwa wanakijiji.

Mfano II:- Katika kijiji cha KILA MTU ANA THAMANI  kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa usafiri hivyo unaweza kuanzisha huduma ya kutoa usafiri wakati huohuo unajitengenezea kipato.

Mfano III:- katika mtaa wa HEKIMA kuna changamoto ya upatikaji wa sehemu ya kula kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TANZANITE YETU hivyo unaweza kuja kufanya biashara ya kuanzisha mgahawa na kuuza chakula kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho na wanajamii wengine.

Mfano IV:- Katika kijiji cha MAARIFA YA MAISHA kuna changamoto ya upatikani wa bidhaa za matumizi ya nyumbani hivyo wananchi wanasafiri umbali mrefu kwenda kununua bidhaa hizo, hivyo basi kupitia chanagamoto hii unaweza kuanzisha baishara ya kuuza duka.

Mfano V:- Katika mtaa wa ELIMU NI MUHIMU  kuna changamoto ya upatikanaji wa mahitaji ya sokoni mfano nyanya ,vitunguu ,matunda n.k hivyo unaweza kuanzisha biashara ya kuuza bidhaa hizo katika eneo zuri na safi ambalo litawavutia wateja kuja kununua bidhaa zako.

MUHIMU 

Tafiti ni muhimu sana kabla ya kuazisha biashara yoyote ile, hivyo basi ninashauri ufanye utafiti wa kina juu ya eneo unaloishi ilikujua changamoto ambazo zinakabili jamii inayokuzunguka na kisha kuja na mpango mkakati wa kuanzisha biashara ambayo inakuwa suluhu ya hizo changamoto wakati wewe unajiingizia kipato.

Itaendelea sehemu ya pili

Imeandaliwa na James Albert 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z