Skip to main content

Ajira Yangu Business Plan Competition


“Ajira Yangu Business Plan Competition” ni mpango mkakati wa kutatua changamoto za ajira kwa Vijana, Tanzania. 
Ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana nchini, Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), kwa pamoja wamebuni mpango huu.
Mpango huu  umebuniwa  kwaajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine pia.

Sote tunajua kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea kama Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira, hali duni ya maisha, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mbinu jumuishi na kukosa fursa za kiuchumi.
Ajira Yangu Business Plan Competition itahusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18-35, wale wanaotaka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao.
Vijana hao watatakiwa kuja na mipango rasimu ya biashara kwaajili ya mashindano katika sekta zifuatazo;
  • Biashara ya Kilimo na kilimo usindikaji ikiwa ni pamoja na viwanda
  • Biashara inayohusu vyombo vya habari, masoko, mawasiliano, michezo, vifaa, sanaa na utamaduni, utalii na burudani.
  • Biashara inayogusa mazingira na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na biashara ya kijamii.
  • Biashara inayohusu habari na mawasiliano, teknolojia  ikiwa ni pamoja na usindikaji biashara
Maombi yataanza kupokelewa kuanzia  Aprili 18  mpaka Mei 9, 2016.
Washindi wa Ajira Yangu Business Competition watatangazwa baada ya majaji kupendekeza majina yaliyokidhi vigezo vilivyowekwa.Washiriki wote watapokea msaada wa kiufundi na kitalaamu ili kukuza biashara zao kwa mwaka mmoja.
Taratibu za Uombaji:
Taratibu za uombaji itahusisha awamu tatu. Awamu ya kwanza itahusisha kujaza fomu ya maombi inayopatikana ndani ya tovuti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC).

Awamu ya pili itahusisha mafunzo ya biashara. Vijana ishirini na tano waliochaguliwa  kutoka awamu ya 1 watapitia mafunzo ya kina kwa siku moja juu ya mipango ya biashara.
Mafunzo haya yatakuwa kwaajili ya vijana wote ishirini na tano waliochaguliwa ili kunoa ujuzi wao katika mipango ya biashara ambayo itasababisha kuendeleza mipango yao ya biashara.
Matokeo muhimu ya mafunzo hayo, itakuwa ni kwa kila mshiriki kuandaa, kuongeza  na kuboresha mpango kamili wa biashara.

Awamu ya tatu ya , Ajira Yangu Business Plan Competition itahitimishwa kwa kuwakutanisha washiriki wote ishirini na tano.
Washiriki ishirini na tano waliochaguliwa watawasilisha mawazo bunifu ya biashara zao mbele ya washauri, majaji, wawekezaji walioalikwa pamoja na wananchi wengine.
Kila mshiriki atapata fursa ya kujieleza kuhusu safari yake ya ujasiriamali na mafanikio yake ya baadaye. Na mchango wa biashara yake katika kujenga ajira kwa wengine.
Baada ya hapo, majaji watachagua mawazo ya biashara iliyo bunifu na yenye uvumbuzi kuliko wote.

Washiriki sita wa kwanza wenye mawazo ya ubunifu watachaguliwa na kila mmoja atapokea tuzo kwa njia ya mtaji ili kuwawezesha kuanzisha au kuendeleza biashara zao, na kujenga ajira zao wenyewe na kwa kwa wengine.

Lengo la Ajira Yangu Business Plan Competition ni kuongeza idadi ya vijana wanawake kwa wanaume katika biashara na kuzalisha kazi na ajira.
Kwa Mawasiliano zaidi:
ILO Country Office, Kazi House, P. O. Box 9212, Dar es Salaam, Tanzania.
Tel : +255 22 2196700 | Mobile: +255 763 160186 | Fax : +255 22 2126627 | Email: lazaron@ilo.org
OR
National Economic Empowerment Council, 12 Kivukoni Street, P.O.Box 1734, Dar es salaam, Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

Hatua tisa za kuanzisha biashara.

Kuanzisha biashara kunahitaji kupanga mipango, kufanya maamuzi ya kifedha  na kutimiza  taratibu kadhaa za kisheria.  Wakati mwingine sio lazima kuzifanya  hatua zote kwa wakati mmoja lakini kadri biashara inavyozidi kuimarika basi ni lazima uzitimize hizo hatua muhimu. Kuna baadhi ya hatua ambazo ni lazima uzifanye mwanzoni kabisa mwa biashara yako, vinginevyo biashara yako itakufa ingali bado changa au itasimamishwa na mamlaka husika za kisheria. Hatua zifuatazo zawaeza kukusaidia katika kupanga,kujiandaa na kuingoza biashara yako kwa ufanisi mkubwa zaidi: Andaa mwongozo wa biashara ( Business plan) Mwongozo huu utakusaidia  kukupa dira ya namna ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Tafuta msaada na mafunzo ya kibiashara Tumia fursa za bure za kujifunza  zinazopatikana mtandaoni au fursa za bei rahisi zinazotolewa katika makongamano ya ujasiriamali na uwekezaji hapa nchini. Chagua eneo sahihi la kuiweka biashara yako. Tafuta us

Mambo muhimu kuhusu mkopo - Sehemu ya 1

            Utangulizi  MKOPO ni kiwango cha fedha ambacho mtu hupewa na taasisi ya kifedha na kutakiwa kurudisha kiwango hicho kikiwa na riba kwa kipindi cha muda fulani. Mkopo unaweza  kuwa katika  mfumo wa bidhaa au kifaa lakini vitu hivyo  vyote hatimaye lazima thamani yake ipimwe na fedha,kwasababu  kazi kubwa ya fedha ni kupima thamani ya bidhaa au vifaa,mfano mtu anapochukua mkopo wa bidhaa zenye thamani ya Milioni kumi,tafsiri  yake ni kwamba umechukua mkopo wa Milioni kumi. Katika makala hii nitaeleza kuhusu mkopo kwa ujumla ingawa kwa sehemu kubwa nitaeleza juu ya mkopo wa fedha  unaotolewa na taasisi za za kifedha. Watu wamezoea kuwa mabenki ndiyo yanayo husika na utoaji wa mikopo tu lakini kiuhalisia kuna taasisi nyingi za kifedha zinazo husika na utoaji wa mikopo . Kulingana na sheria ya benki na taasisi za kifedha vyombo ambayo vinaruhusiwa na huduma ya utoaji mikopo ni benki ,saccos ,makampuni ya mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tafiti zinaonyes

Mambo sita ya msingi kuhusu soko la bidhaa yako au huduma unayotoa

Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu. Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso. Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online). Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri. Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha  kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya. 1.Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa z